NA.GOODLUCK
CHRISTOPHER
Muimbaji
wa nyimbo za injili Tanzania Bw. Heri Mboya
alifanya uzinduzi wa albamu yake mwishoni mwa wiki iliyo pita inayo
fahamika kwa jina la Anajibu maombi , uzinduzi huo ulifanyika katika kanisa la
E.A.G.T Vwawa Mbugani
wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe, Plan Media imemtafuta
Bw.Mboya nae alikua na haya ya kusema “Ninamshukuru Mungu sana uzinduzi ulikua
vizuri mno watu waliofika ni mashahidi walimuona Mungu kwa namna ya pekee”.
Aidha
Mboya amesema aliamua kufanya uzinduzi huo mkoa wa Songwe kwasababu ni nyumbani
aliko zaliwa hivyo aliamua afanyie nyumbani kwanza maana aliona nivyema
kuwaonesha matunda mazuri wale walio
mlea kiroho tangia akiwa mdogo.
Vilevile
amewaasa waimbaji waimbaji wa nyimbo za injili waimbe nyimbo zao katika Roho na
kweli, wakati huohuo ameviasa vyombo vya
habari Tanzania kusaidia muzi huu
kuutangaza kwa nguvu kubwa kama wanavyo fanya kwenye mziki ule wa upande
wapili [muziki wa kidunia].
Albamu
hiyo ni yakwanza kwake kuizindua iko katika mfumo wa DVD ina nyimbo nane ambazo ni Anajibu maombi , Kua uyaone,
Nazisubiri, Wasamehe, Nduna , Nimwema , Usilie na Natembea na yesu. Albamu hii
bado haijapata msambazaji ukiihitaji anakuletea ulipo kwa mawasiliano nitakayo
weka hapo chini.
Pia
amewaomba watanzania ambao ni wapenzi na wasio wapenzi wa mziki wa injili
kununua albamu hiyo ya Anajibu maombi
maana ni nzuri sana na mtu hata jutia kuinunua na kuendelea kumuunga
mkono katika huduma yake,na yuko tayari kwa mialiko anahudumu sehemu yeyote kwa
utukufu wa Mungu.
Hata
hivyo amesema matarajio yake makubwa ni kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na
kwa nguvu zake zote kingali akiwa kijana na akiwa bado ana nguvu za kutosha
kumtumikia Mungu wa mbinguni alie hai.
MAWASILIANO
YA BW. HERI MBOYA
WhatsApp : 0655 174 178 na kumpigia kawaida
Facebook :
@Heri Mboya
Instagram :
@mboyaheri
PICHA
ZA HERI MBOYA AKIWA KWENYE UZINDUZI HUO SIKU YA IJUMA MOSI TAREHE 25/11/2017
TUNAOMBA RADHI KWA MUONEKANO HAFIFU WA PICHI HIZO HAPO JUU ZINAZO MUONESHA HERI MBOYANA WACHEZA SHOO WAKE AKIIMBA KATIKA UZINZUZI HUO MWISHONI MWA WIKI ILIYO PITA.
HIZI NI PICHA BW. HERI ALIZOPIGA NA WENZAKE NJE KIDO YA KANISA LA E.A.G.T VWAWA MKOANI SONGWE ALIPO FANYIA UZINDUZI HUO.










1 Maoni
Safi
JibuFuta