WATUMIAJI wa magari yanayotoa huduma ya usafiri jijijni Dares-salaam[dladala]waliomba jeshi
la Polisi wa barabarani kuwa makini na muda pamoja na kupanga mikakati sahihi
na madhubuti itakayo okoa muda wa watumiaji wa usafiri pamoja na kusaidia
ongezeko la uchumi wa taifa letu.
Wakiongea mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania kwa nyakati
tofuti wasafiri hao wa daladala wamesema ya kuwa kwamba kumekuwa na tabia ya
kusimamishwa kwa magari ya abiria mara kwa mara na wkati mwingine huchukua
takribani robo saa kwa askari hao kumaliza ukaguzi wa basi.
Mmoja wa watumiaji wa daladala hizo aliejulikana kwa jina
moja la Besha amesema kumekuwa na utaratibu usio faa na ambao hauzingatii muda
wa wasafiri kwani huchelewesha watu waendao makazini vilevile hupelekea
kupunguza ama kuchelesha mizunguko ya ruti kwa wafanyakazi wa mabasi hayo na
mwishowe kukosa kipato cha kuridhisha.
Vilevile mwandishi wa gazeti hili alipata kumhoji mmoja wa
Dereva wa daladala zifanyazo safari zake Gongo la Mboto Makumbusho ambae
hakupenda jina lake lifahamike alisema kuwa ni kweli wanakuwa na makosa katika
mabasi yao lakini tatizo ni pale wanapokuwa wanakamatwa mara kwa mara na askari
tofauti jambo ambalo hakubaliani nalo na badala yake ameliomba jeshi la polisi kuweka
utaratibu sahihi wa kudhibiti magari mabovu.
Ikumbukwe kuwa mapema katika uongozi wa awmu ya tano
umewekwa utaratibu mzuri ambao unatumiwa na jeshi la polisi wa barabarani,ambao
utaratibu huo ni wa kumuandikia kosa pamoja na kulipia kupitia max
malipo,ambapo utaratibu huo ni mzuri na umesaidia kutunza muda kwa watumiaji wa
usafiri wa daladala.

0 Maoni