NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Muimbaji
wa nyimbo za injili Tanzania Bw.Mecracy Bukulu amesema kuwa sababu kubwa inayo
wafanya waimbaji wachanga wa nyimbo za injili Tanzania kuto kujulikana kuwa ni udhamini katika nyimbo hizo kuwa mdogo ukilinganisha
na muziki wa upande wa pili yani bongo freva.
Aidha
Bukulu amesema kuwa mbali na waimbaji
hao kujulikana makanisani kwao inakua
changamoto kubwa kujulikana sehemu kubwa kwasababu walio wengi hawana pesa
yakutosha kutangaza huduma yao nje ya makanisa wanayo Sali kwa maana ya kutumia
vyombo vya habari pamoja na matamasha mbalimbali na hatimae wanaishia
kujulikana ndani ya makanisa wanayo Sali.
Vilevile
Bukulu amesema kuwa wasambazaji wa
nyimbo za injili Tanzania ni wachache ukilinganisha na idadi ya waimbaji wa
nyimbo hizo kwasasa, hivyo wanawatoza gharama kubwa kuzisambaza nyimbo hizo
jambo ambalo waimbaji wachanga hushindwa kumudu gharama hizo.
Pia
Bukulu amewaomba watu wenye uwezo na makampuni kuwekeza katika kasambaza kazi
za waimbaji wa nyimbo za injili pamoja na kudhamini katika matamasha mbalimbali
kama ilivyo katika muziki wa upande wapili yaani bongo freva lengo ikiwa ni
kuitamgaza injili kamili ya Yesu kristo kwa watu wote.
Bukulu
amemalizia kwa kutambulisha wimbo wake mpya ambao uko katika mfumo wa audio
inayo inayo itwa Yesu ni mzuri “Natambulisha wimbo wangu mpya [audio] ya Yesu
ni mzuri na imeanza kupokelewa vema na wasikilizaji wa media za gospel
Tanzania” mwisho wa kunukuu.


0 Maoni