NA.
MWANDISHI WETU
Marekani imeyataka
mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea
Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja
wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa
rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa
Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea
Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia
majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo
lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475,
ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.
Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam
wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.
Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong
Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.
Jaribio hilo likiwa mojawapo ya majaribio
yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza
la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.
Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi
kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.
''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'',
alisema Rais Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano ,
Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu
akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi
na kusitisha mpango wake wa kinyuklia.
SOURCE. BBCSWAHILI.COM


0 Maoni