NA.MWANDISHI WETU
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu
katika serikali yake.
Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali
aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi
limechukua udhibiti.
Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri
ataongoza wizara ya fedha na kilimo.
Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema
kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.
Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita
kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban
miaka saba.
Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti
wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama
vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti
taifa hilo.
Hali ya kuleta uwiano na umoja ilioonekana
katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika
uchaguzi wa mwaka ujao.
SOURCE. BBCSWAHILI.COM



0 Maoni