NA.MWANDISHI WETU
Mwanamume
mmoja amelipua maguruneti mawili katika mahakama moja mashariki mwa Ukraine ,
akijiua pamoja na mmoja wa washukiwa wa mauaji ,kulingana na maafisa wa polisi.
Mlipuko huo ulitokea wakati wa kikao cha
kusikizwa kwa kesi hiyo mjini Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk.
Mtu huyo ni baba ya mmoja wa waathiriwa
waliouawa kulingana na maafisa wa polisi.
Takriban watu tisa walijeruhiwa, ikiwemo
washtakiwa wawili , walinzi wawili afisa mmoja wa mahakama na raia.
Washtakiwa hao watatu wanatuhumiwa kuifyatulia
risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016 akiwemo
mwana wa mtu ambaye alilipua vilipuzi hivyo , kulingana na vyombo vya habari.
Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja alitoa
maguruneti mawili na kuyalipua wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji kulingana
na mtandao wa Ukrainska Pravda ambao ulimnukuu msemaji wa polisi Yaroslav
Trakalo akisema.
Mtu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kusikia
kwamba kesi hiyo inaahirishwa na kwamba washukiwa wanafungwa mikono.
Uchunguzi sasa umeanzishwa.
Mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine
unamaanisha kwamba kuna umiliki wa silaha miongoni mwa raia.
Zaidi ya watu 10,000 wamefariki katika mzozo
huo uliotokea mnamo mwezi Aprili 2014, muda mfupi baada ya Urusi kulinyakua
eneo la kusini la rasi ya Crimea.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni