NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Kanisa
la FPCT lililopo Kihonda Maghorofani
Manispaa ya Morogoro limezinduliwa rasimi leo kuwa kanisa la mahali , uzinduzi
huo umefanyika katika viwanja vya kanisa hilo katika kata ya kihonda wilaya ya
morogoro mjini [manispaa].
Aidha
uzinduzi huo umeambatana na kuwasimika viongozi wapya wa kanisa hilo ambao ni
mchungaji mkuu wa kanisa hilo ambe ni Ndugu. Wilbert Lwambae, mchungaji
msaidizi ambae ni Ndugu. Vicent Msaki pamoja na watenda kazi wengine katika
idala mbalimbali zinazo patikana kanisani hapo.
Mgeni
rasimi ni Mhungaji.Profesa Phill ambea
ameahidi kutoa kiasi cha pesa za kitatanzania milioni moja kwaajili ya kusaidia
ujenzi unao endelea katika jingo la kanisa hilo pamoja na ofisi mpya ya
mchungaji.
Vilevile
kanisa hilo limezinduliwa kuwa kanisa la mahali kutoka palishi ya ukumbi wa
mfalume sulemani ambayo ilikua chini ya kanisa la FPCT magereza, hivyo kuzundiliwa
kuwa kanisa la mahali kihonda maghorofani kanisa hilo litakua likijitegemea.
Pia kanisa hilo lilianzishwa mnamo mwaka 1962
likiwa na waumini wapatao 8 na mpaka sasa lina waumini wasio
pungua 6000 na kufikia mwaka huu 2017 kanisa hilo limefanikiwa kuwa na palishi
zisizo pungu kumi.
Hata
hivyo wageni kutoka palishi zingine, baadhi ya viongozi wa serikali, waasisi wa
kanisa hilo pamoja na viongozi wa makanisa mengine walio alikwa walipata
kuhudhulia sherehe hizo.
Vilevile
kanisa hilo linaendelea na ujenzi ambapo jengo hilo limeisha kwa asilimia 73
likiwa limegharimu kiasi cha pesa za kitanzania milioni 43 zikiwa zimesalia
milioni 37 kukamilisha milioni 80 zinazo
kadiriwa kuwa kutamaliza jengo hilo.
KWA PICHA ZAIDI ZA UZINDUZI HUO HIZI HAPA CHINI.
Picha zote zilizopo hapo juu zinamuonesha mgeni rasimi Mch. Profesa Phill.
Viongozi wakimsindikiza mgeni rasimi akiingia ndani ya kanisa mara baada ya kukata utepe.
Muonekano wa ndani ya kanisa hilo la FPCT kihonda Maghorofani








0 Maoni