NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
Mujimbaji
wa nyimbo za injili Tanzania anae fanya
vizuri kwa sasa Betha Mwafilombe
amezungumzia ujio wa albam yake mpya ya kwa
neema tu
kuwa imepokelewa vyema na wadau wa muziki wa ijnili hapa Tanzania zaidi ya
alivyo dhania kuwa itapokelewa hivyo.
Aidha Betha
amesema kuwa albam hiyo yenye nymbo nane inafanya vizuri sana kwasasa katika
ulimwengu wa injili hapa nchini huku albam hiyo ikichezwa na vituo vingi vya
radio na wasikilizaji wa radio hizo wameonesha kuzipenda nyimbo hizo.
Vilevile Betha hajapata msambazaji wa kuisambaza albam
hiyo ili iwafikie watu wa mikoa ya mbali na mkoa wa Dar es salaam hivyo
anahitaji msambazaji wa kuweza kuisambaza albam hiyo maana anatamani ifike kila
kona na kila anae ihitaji aipate.
Albam
hiyo inapatikana kwa kiasi cha Tsh. 5000/= Tuu. Mtu ane ihitaji kwasasa
anakuletea mwenyewe mali ulipo kupitia mawasiliano nitakayo kuwekea hapo chini
na wale wa mikoani amesema kuwa anawaagizia kwa njia ya mabasi na inakufikia
popote ulipo.
Pia
Betha amesema yuko tayari kwa mialiko na yupo tayari kutumika mahali popote kwa
utukufu wa Mungu hivyo kwa watu wa mikoani na nje ya nchi wawe huru kumualika
makanisani, mikutano na matamasha hato sita kufika kwa utukufu wa Bwana.
Betha
amesema kuwa uzinduzi wa albam hii utafanyika viwanja vya Mababu CCM wilaya ya Kyera mkoani Mbeya
tarehe 7/7/2018 amewaomba wadau wa mziki wa injili kujitokeza kwa wingi siku
hiyo.
Hata
hivyo betha amemaliza kwa kusema kuwa video ya albam hiyo inatarajiwa kufanyika
mwaka u8jao wa 2018, hivyo wadau na wasio wadau wa muziki wa injili wajipange
kuipokea video nzuri na yenye ubora wa hali ya juu mapema hapo mwakani.
MAWASIILIANO YA BETHA
HOTLINE: 0767 406 265
INSTAGRAM: BETHA J MWAFILOMBE
FACEBOOK. BETHA J MWAFILOMBE


0 Maoni