Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko nchini Saudi
Arabia katika ziara isiyopanga, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini
Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo.
Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya
Rais Macron imekuja siku moja baada Waziri mkuu Saad Hariri, kujiuzulu wakati
alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia.
Awali akizungumza mjini Dubai, Rais Macron amesema anataka
viongozi wa Lebanon kuishi huru ndani ya nchi yao.
Amesema pia atautaka uongozi wa Saud Arabia kusaidia kuzuia baa
la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo
yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa
Ki Houthi.
SOUCE . BBCSWAHILI.COM


0 Maoni