Rais Donald Trum wa Marekani amesema kuwa Marekani haitavumilia
biashara yenye upendeleo, katika hotuba yake iliojaa malalamishi katika mkutano
wa mataifa ya bara Asia na yale yaliopo katika bahari ya Pacific{Apec} mjini
Vietnam.
Amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec
iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote.
Bwana Trump alisema kuwa biashara huru iliathiri kazi za
mamilioni wa raia wa Marekani na sasa anataka usawa kutekelezwa.
Tayari ameitembelea China na Japan katika zaira yake ya mataifa
matano ya bara Asia.Apec unaleta pamoja uchumi wa mataifa 21 kutoka eneo la
Pacific ambao ni asilimia 60 ya uchumi wote duniani.
Tangu achukue mamlaka rais Trump ameiondoa Marekani katika
muungano wa Trans-Pacific, ambao unahusisha mkataba mkubwa wa kibishara
unaoshirikisha mataifa 12 ya Apec akidai kwamba utaathiri uchumi wa Marekani.
Katika hotuba yake siku ya Ijumaa rais Trump alilishutumu
shirika la biashara duniani WTO ambalo hutengeza sheria za biashara duniani na
kusema haliweza kufanya kazi zake vyema iwapo wanachama wake hawataheshimu
sheria hizo.
Alilalamika kuhusu ukosefu wa usawa wa kibiashara akisema
Marekani imeondoa vikwazo vya kibishara huku mataifa mengine yakikataa kufanya
hivyo.
''Vitendo kama hivyo vinaathiri watu wengi katika taifa langu'',
aliwaambia viongozi wa kibishara na wale wa kisiasa katka mkutano huo.
Lakini hakuyalaumu mataifa ya Apec na badala yake kulalamikia
watawala wa awali wa Marekani kwa kutoingilia swala hilo na kurekebisha hali.
SOURCE. BBCSWAHILI.COM


0 Maoni