NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya
Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu
wa kabila la Wazanaki.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya
babake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi
katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.
Baada ya kumaliza
shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko
Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki
hadi mwisho wa maisha yake. kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila
kitu ya Nyerere, Mapadre wa Kanisa katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri
ya kutaka kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha
Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.akiwa katika Chuo cha
Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia akaamua
kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi
Tabora akifundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s), Mwaka
1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko
Uskoti / Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua
hiyo Mwalimu alikuwa mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha
Uingereza na mtanganyika wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya
Tanganyika. Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha
Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na
Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari).
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha
Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa
mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha
TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho
kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU
kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika. Uwezo wa mwalimu
uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa
na kazi ya ualimu.
Nyerere alisikika
akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. aliamua
kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida
na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa
niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya
Umoja wa Mataifa (UN) huko New York Marekani. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu
ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull,
ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni
mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika
ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa
Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa
jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa
Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar
mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977,
aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar
ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti
wake.
Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong,atuka
na kumwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea
kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na makini na mfuatiliaji huku akionya
katika mambo kadhaa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. baada ya kustaafu
kazi ya ukuu wanchi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa
Butiama akilima shamba lake la mahindi.
Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina
lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation, mwaka 1996 alionekana
akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko
Burundi. Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida
kijijini kwake Butiama Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka
1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara baadaye alihamishiwa katika
Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.
Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali
hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu (
leukemia). Mafanikio na kasoro Kitendo kikubwa ambacho hakisahahuliki ambacho
Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka ni kuchanganya ardhi za Zanzibar na
Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi
leo upo.
Kujenga umoja wa kitaifa
na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa
rangi, kutetea usalama wa taifa katika vita dhidi Nduli Idi Amin Dada wa
Uganda. watu walimuita mwalimu kuwa ni mwanamapinduzi wa afrika, kiongoiz wa
bara zima kutokana na nia zake za kutaka kila Mwafrika kuwa huru na kuwa na
amani.
Mwalimu pia alifanikiwa kutoa mchango kwa
vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika
Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (FRELIMO)
Kutofanikiwa kwake Kitu ambacho kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara
nyingi ni juu ya kutofanikiwa kwa nia yake ya kuanzisha siasa za Kijamaa.
Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya
mwaka 1976. Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa
za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa
muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais
baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani kwa Mwinyi aliyetawala kwa
siasa za uchumi wa soko huria. Katika hali ya kukubali ukweli,
Nyerere alitamka katika tafrija ya kumwaga juu
ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.” Alikosolewa pia Kutokana na
hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa
siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania,
Pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo wao
yanazitamani siasa hizo.
Pia kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa
kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa
wakristo. Kutangazwa mwenye Heri Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa
kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa
hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa
mwenyeheri, Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu.
Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu
na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu.
Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa
na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu Justine Samba. Alikuwa
mwanamichezo Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wan
chi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo, alianznisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama
alicheza bao nyumbgani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa
na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.
Kutokana na maisha yake aliyoyaishi ambayo
yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa
wa hali ya chini hasa kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu. Ni
mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na
kutawala kwa miaka zaidi ya 24. Taifa linamkumbuka kwa hayo na mengi ambayo
aliyafanya, ameacha machapisho mengi ambayo pia yamekuwa hazina ya maarifa kwa
watanzania


0 Maoni