NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Betha
alizaliwa tarehe 2/2/1996 katika kijiji cha Mababa wilayani Kyela mkoani Mbeya
ni mtoto wa saba na wamwisho katika familia ya watoto saba wa mzee Jonathani
Mwafilombe, Betha ni muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania pamoja na sauti
nzuri aliyo jaliwa ya kuimba pia anauwezo wa kuandika mashairi ya nyimbo za
injili kwa maana nyingine ni mtunzi na muimbaji wa nyimbo za injili.
Mnamo
mwaka 1997 familia yake ilihamia Kinondoni shamba mkoani Dar es salaam kipindi hicho akiwa na
umri mdogo umri wa mwaka mmoja, Betha alishi hapo na wazazi wake katika makao
mapya na maisha hayo huku umri ulizidi
kusogea.
Mnamo
mwaka 2004 akiwa na miaka 8 alijiunga na shule ya msingi Kumbukumbu Kinondoni
B, Betha hakubahatika kupata elimu ya awali yaani chekechea na badala yake
alijiunga mojakwamoja na darasa la kwanza katika shule hiyo kutokana na umri
alio kuwa nao kwa kipindi kile .
Mnamo
mwaka 2006 akiwa daresa la tatu familia ilirudi tena mkoani mbeya hinyo
ilimlazimu kuhama shule akaomba uhamisho walipo fika mbeya akajiunga na shule
ya wamsingi Mababu katika kijiji cha
Mababu wilayani Kyela akaendelea na darasa la tatu akaendelea kupata elimu
katika shule hiyo.
Mnamo
mwaka 2010 alihitimu elimu ya msingi kwa maana ya daresa la saba katika shule hiyo ya msingi
Mababu hapo alikua na umri wa miaka 16, Betha hakuweza kufanya vizuri katika
mtihani wake kitu kilicho fanya wazazi wake kushindwa kumsomesha katika shule
binafsi maana kipato chao kilikua hakikidhi kumsomesha katika shule hizo hivyo
safari yake ya kielimu iliishia pale.
Mnamo
mwaka 2011 Betha aliamua kuokoka katika kanisa la Luthelani[KKT] Mababu mkoani
Mbeya na safari yake ya wokovu ilianzia pale ndipo alijiunga na kwaya ya kanisa
hilo ambapo alitumika katika kwaya hiyo ndani ya mwaka mmoja.
Mnamo
mwaka 2012 alianza kuandika ama kutunga nyimbo zake na kuanza kuingia katika
studio ya John Joram ambapo alipata
kurekodi nyimbo tatu ambazo ni 1:Kwa neema
2:Siku za mwanadamu 3: Mambo mengi richa ya kurekodi nyimbo hizo bado
alipata changamoto ya ubora wa nyimbo hizo ambao haukuwa mzuri.
Mnamo
mwaka 2014 alirudi jijini Dar es salaam huku akiwa na changamoto ya sehemu ili
aishi wakati akitafuta studio nzuri, Betha alifanya mawasiliano na mama mkwe wa
dadayake ndipo alipo fikia maeneo ya kinondoni shamba jijini Dar es salaam akakubaliwa
anaishi hapo.
Mnamo
mwaka 2015 Betha alimpoteza babayake mzazi mzee Jonathani Mwafilombe ilikua tarehe 5/2/2015 ambae
alikua akisumbuliwa na tatizo la vidonda vya koo vilivyo pelekea umauti wake
jambo hili lilimfanya Betha asikitike kwani babayake alikua ndie nguzo yake
katika kila alifanyalo hata hivyo alichukulia tukio lile kama changamoto ya
maisha kwakua imeandikwa kila nafsi
itaonja umauti hivyo aliendelea na huduma yake ya uimbaji.
Mwaka
huu wa 2017 aliingia katika studio ya Ommary Mkali iliyopo iliyopo Mbezi Ruisi
jijini Dar es saam akapata kuboresha nyimbo zile tatu alizo zirekodi kwa John
Joram studio mbeya pamoja na kuongeza nyimbo
tano ambazo zinatimiza nyimbo nane kwa sasa
nazo ni 1:Kwaneema, 2: Siku za
mwanadamu, 3:Mambo mengi, 4:Hasira
hasara, 5:Mali za ulithi, 6:Mwacheni Mungu aitwe Mungu 7:Pigo la mama 8:Ume mwasi Mungu ambazo kwasasa zinafanya
vizuri na zinachezwa katika vituo mbali mbali vya radio hapa Tanzania.
Richa
ya Betha kuwa muimbaji wa nyimbo za injili pia ni mjasiliamali ambae analima
kilimo cha mboga mboga na matunda pamoja na ufugaji wa mifugo aina ya Nguruwe
mkoani Mbeya ambavyo humuingizia kipato na kumsadia kufanya shughuli mbali
mbali ikiwemo kujilipia gharama za kurekodi nyimbo zake
MAWASILIANO
YA BETHA
SIMU.
076 740 265
FACEBOOK. BETHA J MWAFILOMBE
INSTAGRAM.
BETHA J MWAFILOMBE
Huu
ndio mwisho wa wasifu wa Betha Jonathani
Mwafilombe tutaendelea kuwaletea wasifu wa watu wengine hivyo usikose
kutembelea PLAN MEDIA kwa mambo mengi na mazuri. Asanteni.
Kama
unahitaji kuandikiwa wasfu wako kama Betha wasiliana nasi kwa:
+255713
305 650
planmediatz@gmail.com


0 Maoni