NA.
GOODLUCK CHRISTOPHER
Wakatikati kati ya hao wawili ndie Mh. Fred Peter Iske ambae ameji hudhuru nafasi hiyo kwa sasa picha na Maktaba. Tunaomba radhi kwa muonekano usio ridhisha.
Raisi
wa serikali ya wanafunzi TSJOSO katika chuo cha uandishi wa habari Time School
of Journalism [TSJ] kilichopo Ilala jijini Dar es salaam Mh. Fred Peter Isike ajihudhuru nafasi ya uraisi katika chuo
hicho leo hii.
Aidha
Isike ametoa kauli hiyo katika viwanja vya chuo hicho mala baada ya kipindi cha
redio kwa vitendo ambacho hufanyika kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa nane na
dakika hamsini mpaka saa kumi kama ilivyo pangwa na uongozi wa chuo hicho.
Vilevile
Isike hajatoa sababu mahususi zilizo mfanya kuachia ngazi hiyo na badala yake
amesema leo hawezi zungumza chochote kuhusiana na uamzi huo na kuongeza kusema
kwamba atabakia kuwa mwanachama wa kawaida katika serikali hiyo ila
atazungumzia uamzi huo siku nyingine ambayo hajaitaja.
Kwa
upande wa mwalimu mlezi wa wanafunzi chuoni hapo Bw. George Bartazal alipokea
uamzi huo kwa masikitiko makubwa na kusema kuwa haijawahi kutokea katika chuo
hicho kwa raisi kujihudhuru hivyo imemshangaza sana kuona uamzi kama huo.
Gerge
amempongeza isike kwa ujasiri alio uonesha kwasababu ni uamzi mgumu ambao si
rahisi kwa mtu mwingine kuufanya na
kusema kuwa kunawatu wengine hulewa na madaraka lakini wengine pia uongozi ni
sehemu inayo wafanya wajifunze jinsi ya kuishi na watu.
Pia
George amesema kuwa Isike kabla ya kujihudhuru
nafasi hiyo alipokea barua ya kujihudhurukwa kiongozi ikisema kwamba
ameamua mwenyewe bila kushurutishwa wala kushauriwa na mtu kuchukua uamzi huo
hivyo ameadhimia mwenyewe.
Aidha
George ametangaza kuwa kuanzia leo chuo hicho hakina serikali na badala yake
akaamua kutangaza kwa wanafunzi wanao jiona kuwa wana uwezo wa kuwa viongozi
kugombea nafasi mbalimbali katika serikali hiyo ambapo kampeni zitafanyika kwa
muda mfupi zaidi kwa sababu ni uchaguzi mdogo hivyo haoni haja ya kusubiri siku 30 za kuitisha uchaguzi huo kwa mjibu wa
katiba wakati kuna wanafunzi wanao tazamia kuanza mitihani hapo Novemba13 na
kusema anataka wanao hitimu wasikiache chuo kikiwa hakina serikali .
Vilevile
Gerge amewataka wanawake kuamka na kugombania nafasi mbalimbali na si kuwaachia
wanaume kugombania nafasi hizo pekee kwasababu wanawake nao wana uwezo mzuri wa
kuiongoza serikali hiyo na kutoa msemo huu
“ukiona mafanikio ya mwanaume ujue kuna mwana mke nyuma yake”.
Pia
George amemteua Bw. Abdallah Twaha kuwa
mwenyeki wa tume ya uchaguzi uanao tarajiwa kufanyika hivi karibuni na kumuita
mbele ya wanafunzi achague kukubali au kukataa kuendesha tume hiyo Twaha amekubali
kwa kiapo hiki ‘’mimi Abdala Twaha kwa
heshima niliyo pewa kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mdogo kwa akili yangu
timamu bila kushurutishwa nimekubali’’


0 Maoni