Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

HATUA TANO ZA KUANZISHA BIASHARA YEYOTE

NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
BIASHARA, Tafsiri ya neon biashara kisomi ni kuuza na kununua bidhaa hivyo ili kuwe na kitu biashara basi  ujue kuna mtu anahitaji bidhaa na analipa kitu Fulani ili kupata kitu hicho na malipo yenyewe yana weza yakawa ni pesa au bidhaa tofauti na ile anayo hitaji.

Tukirudi nyuma kidogo kulikua hamna pesa hivyo walilazimika kufanya biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa kwa mfano ukihitaji Mahindi kwangu unanipatia Maharage waliishi hivyo tofauti na sasa ambapo biashara kubwa ni bidhaa kwa pesa.

Katika somo la leo tutajifunza zaidi biashara ya kuuza bidhaa na kupewa pesa kulingana na karne hii ya 21 ambapo biashara iliyo shamiri ni ya malipo ya pesa ili kujipatia bidhaa unayo ihitaji.

Biashara ni suala pana sana kitaka ulimwengu  na biashara ni sehemu ambayo imebeba ajira za kuwatengenezea kipato cha kuendesha maisha ya watu wa aina zote kwa maana ya watu wenye uwezo wa hali yajuu, kati na chini hii inaonesha ni jinsi gani biashara imeshikilia maisha ya watu wengi duniani.

Kuna mataifa yaliyo endelea kibiashara kwa kiasi kikubwa kama nchi ya Marekani ambayo biashara  kwasasa pesa yake ni ya dunia hii inaonesha ni kwa kiasi gani nchi hiyo iko vizuri kibiashara huku nchi ya Tanzania ikiwa katika uchumi wa kati hivyo kuna haja ya kuongeza juhudi kuufikia uchumi wa juu.

Kutokana na watu wengi kujiingioza katika suala zima la biashara kuna watu ambao hufanikiwa kwa kiasai kikubwa huku wengine wakishindwa kufanikiwa na tatizo kubwa ikiwa ni kujiingiza katika biashara bila elimu ya kutosha maana biashara nayo inahitaji elimu kama kazi nyingine yeyote.

Kuna mambo mengi ya kuzingatia katika kuanzisha biashara yeyote na kupitia makala hii tutajifunza mambo matano mhumu ambayo mfanya biashara anapaswa kuyazingatia ili kunufaika na biashara hiyo anayo ifanya.

 Mambo matano tunayo jifunza leo hii ni haya hapa chini panapo majaliwa nitakuletea somo jingine ambalo tutapata kujifunza kiundani zaidi chamsingi ni kutembelea [PLAN MEDIA] marakwamara kwa elimu zaidi.

1:Huenda ukawa umegundua kuwa kuna mawazo au aina milioni moja za biashara, lakini ukachagua wazo moja tu, ambalo hilo utakuwa umefanya maamuzi magumu na yapekee kulipa kipaumbele. Japokuwa haina haja ya kulipa kipaumbele wazo moja tu na kuliona ndilo la pekee katika kuanza biashara.
2:Wazo lolote lile la biashara ulilochagua, ningependa kukushauri kuwa usianzishe biashara ambayo ni maarufu kwa wakati huo, biashara ambayo inafanywa kwa kiasi kikubwa na wafanya biashara walio wengi. Ukifanya hivyo utawanufaisha wafanya biashara wakubwa kwanza halafu wewe utakuwa wa mwisho.
3:Wazo lako la kuanzisha biashara yako, ni lazima litokane na sehemu ya shughuli zako ambazo tayari ni sehemu ya maisha yako, shughuli ambazo tayari unazifurahia kuzifanya kila kukicha. Unapaswa kufanya kitu unachokipenda kutoka moyoni, kitu ambacho kinakufurahisha kila kukicha.
4:Pia unatakiwa kujifunza mengi zaidi kuhusiana na wazo lako la biashara uliloliteua. Lifanyie utafiti wakutosha, kwani unavyozidi kujifunza mengi, ndivyo unazidi kuwa mzoefu katika kuanzisha biashara yako. Ukifanya hivyo utaanza biashara yako ukiwa na uzoefu wa hali ya juu na mafanikio yatakuwa upande wako siku zote.
5:Kitu muhimu: Wazo lako la kuanzisha biashara  lazima liendane na mahitaji ya wateja au wanunuzi. Endapo kama haliendani au kukidhi mahitaji ya watu, basi hakuna mtu atakaye kuja kununua bidhaa yako au huduma yako. Hivyo fanya kwanza utafiti kabla ya kuanza. Hakikisha unafanya utafiti wa mahitaji ya wateja, hata ikiwezekana waulize watu wa eneo hilo mahitaji wanayohitaji kununua ndipo uanzishe biashara yako.

Biashara ina umhimu mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu kwasababu dunia ynyewe inaendeshwa kwa mfumo wa kibiashara na kila unacho jaribu kufanya unakuta kinaingia katika suala la biashara hata kama hupendi iwe hivyo itakulazimu kuendana na mfumo wa dunia ya ki biashara.
Mwisho kabisa, katika dunia hii asikwambie mtu, biashara ni matangazo, bila matangazo ni sawa na bidhaa bila mnunuzi. Fanya hima tangaza biashara yako katika vyombo mbali mbali vya habari, utaona manufaa ya kazi ya yako, kwa kutambua hili ndio mana plan media tukatoa ofa kubwa ya matangazo.
TANGAZA NA PLAN MEDIA & TV
CONTACT: 0713 305 650

 







Chapisha Maoni

0 Maoni