NA. MARYAM MMAMBIYA
Wananchi wa Yombo
kilakala wilayani Temeke waitaka serikali kuongeza magari ya kuzelea taka ,
haya yameongelewa na wananch hao baada ya uchache wa magari hayo jambo linalo
pelekea mrundikano wa takataka na
kusambaa katika makazi ya watu baada ya sehemu iliyo andaliwa kukusanyia taka kufurika
wingi wa taka hizo.
Aidha mmoja wa wananchi hao Bi. Sabrina Komba ameiambia plan
media kuwa ukosefu wa magari hayo unasababisha uchafuzi wa mazingira kwa kiasi
kikubbwa hususa ni katika kipindi hiki
cha mvua nyingi ambapo maji hubeba taka hizo na kuzisambaza katika makazi ya
watu na zingine huingia katika mto yombo ambapo husafirishwa moja kwa moja
mpaka baharini.
Vilevile Bi. Sabrina
mesema afya za wakazi hao ziko hatarini kutokana na uchafu huo ambao unaweza kusababisha magojwa ya mripuko na
kupoteza maisha ya wakazi hao hususa ni watoto wadogo wanao cheza michezo yao
katika maeneo hayo.
Kwa upande wa
mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Juma Matari amekiri kuwepo kwa uchafu huo na kudai
kuwa magari yamekua ni changamoto kubwa
sana hivyo wapo katika mchakato wa kulitokomeza tatizo hilo na hivi karibuni
hali itakua swari na wananchi wataishi kwa amani na afya zao zikiwa njema.
Pia Matari
amewata wananchi hao kuwa watulivu katika
kipindi hiki kigumu na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha tatizo hilo
lina tokomea kabisa ili wakazi waishi katika mazingira masafi na salama kwa
afya za wakazi hao.
Hata hivyo suala la
usafi wa mazingira limekua changamoto katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
es salaam hususa ni katika kipindi hiki cha mvua jambo ambalo linaleta wasiwasi
kwa afya za wakazi waishio katika jiji la Dar ea salaam kwa ujumla.
Richa ya mkuu wa mkoa
Mh. Paul Makonda kuteua siku ya jumamosi kuwa siku ya usafi katika maeneo yote
ya jiji la Dar es salaam siku hiyo imekua haizingatiwi katika baadhi ya maeneo
na ndio maana tunaona maeneo mengi yakiwa machafu sana hususa ni katika masoko
kama; Buguruni,Tandika, Tandale n.k




0 Maoni