NA. MARYAM MMAMBIYA
Wanaichi wa Yombo
wilani Temeke jijini Dar es salaam wachoshwa na vitendo viovu wanavyo fanyiwa
na kundi la vijana wanao jihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya
bangi,wananchi hao wameiambia plan media kuwa wamekua wakiporwa malizao
ndogondogo kama simu,pesa pamoja na mikoba wakati mwingine kuibiwa nguo zilizo
anikwa kwenye kamba.
Wakizungumza kwa na
plan media kwa nyakati tofauti walikua na haya ya kusema; Bw. Peter John ambae
ni mkazi wa eneo hilo amesema huwa anaporwa simu ya mkononi wakati mwingine
pesa au viatu na vijana hao nyakati za jioni akitoka katika shughuli zake za
kujitafutia kipato
.
Pia Peter ameongeza na
kusema kuwa vijana hao wanatumiza zana hatarishi kwa maisha ya binadamu kama
visu, nyembe na misumari ambayo hutumia katika kupora mali hizo na mtu anapo
nga’ang’ania kuwapa wanavyo vihitaji wana mjeruhi na zana hizo hivyo watu wengi huwa waoga na
kuwapatia vitu hivyo wanavyo kuwa
wakivihitaji vijana hao.
Vilevile mmoja kati ya
wavuta bangi ambae hakupenda jina lake
liandikwe amesema kua si kila mtu anae vuta bangi ni mkabaji wa mali ndogondogo
bali ni baadhi wasio jitabua wanao fanya hivyo jambo ambalo linafanya jamii
iwachukulie hivyo bali wengine wanavuta bangi kwa kujiburudisha kama wengine
wanavyo kunywa pombe.
Hata hivyo polisi
wamekua wakijitahidi kufanya doria na kuwakamata baadhi yao na kuwaweka ndani [jera] baada ya siku kadhaa wanatolewa nje ,richa ya
polisi kufanya hivyo bado vijana hao wanaendelea na tabia hiyo ambayo ni kero
kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Pia wakazi hao
wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwakua ni hatari kwa maisha
ya wakazi hao kwasababu lisipo tatuliwa
mapema litaathiri kizazi kijacho kwa ujumla hivyo ni vyema kuilitokomeza tatizo
kabla halijawa kubwa zaidi.
Tatizo la matumizi ya
dawa za kulevya limekua ni tatizo linalo pigiwa kerere na viongozi wakubwa wa
serikali na dini lakini bado linaendelea kuwaathili vijana wa kitanzania richa
ya kupigiwa kerere kwa kiasi kikubwa pengine elimu inahitajika kwa kiasi kikubwa.
Dawa za kulevya
zinapunguza nguvu kazi ya taifa hususa ni kwa vijana ambao ni taifa la leo na
taifa bila vijana haliwezi kufika popote wazazi
pamoja na viongozi ni wakati wa kupeana ushirikiano katika kutatua
tatizo hili na sio kuwaachia wana siasa hili ni tatizo la kutatua wote kwa
ujumla.


0 Maoni