NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
Wakazi na watumiaji wa
barabara inayo unganisha Buguruni kwa mnyani na Vingunguti machinjioni jijini Dar es salaam wapaza sauti zao baada
ya kukutana na kamera ya Plan Media wakilalamikia ubovu wa barabara hiyo na
kuiomba serikali kuiboresha barabara hiyo ambayo imegubikwa na ubovu kwa muda
mrefu pasipo kuikarabati.
Aidha barabara hioyo ina mashimo
mengi pamoja na kujaa maji katika mashimo hayo kutokana na mvua zinazo endelea
kunyesha jambo ambalo linasababisha wananchi hao kuitumioa kwa taabu na
kusababisha foreni ya magari amboyo huwasababishia watu kuchelewa katika safari
zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
baadhi ya wananchi hao walikua na haya yakusema, Bw. Shaaban Songo ambae ni
kondakta wa gari la abiria linalo fanya safari zake kati ya Vingunguti na
Mnazimmoja amesema barabara hiyo imekua kero sana ambapo husababisha magari yao
kuharibika marakwamara kutokana na mashimo ya barabara hiyo.
Vilevile Bi. Maryam Marwa ambae ni mkazi wa Vingungunti
dereva wa gari binafsi amesema wanalazimika kubuni njia za vichochoroni wakihofia kuharibika kwa magari yao huku wakiingia garama kubwa ya mafuta
pamoja na muda kwasababu huwapasa kutembea taratibu sana.
Kwa upande wa Bw.Hasheem Mhina ambae pia ni mkazi na mfanya
biashara wa vingunguti amesema wanapata shida kupitisha mizigo yao kwa kutumia
magari makubwa ya mizigo wakihofia kuzama kwa magari hayo kwasababu ubovu huo
unatisha mno.
Pia Bw. Husien Mpilaru ambae ni
serikali ya mtaa amesema anafahamu ubovu wa barabara hiyo na kuiambia plan
media kwamba babara hiyo haiko chini ya manispaa ya ilala bali ipo chini ya
TAKULA ambao walitakiwa waitengeneze tarehe 5/10/2017 huku mpaka leo hakuna
dalili za TAKULA kuitengeneza barabara hiyo.
Vilevile Mpilaru ameongeza na kusema
kuwa anaiomba serikali kuja kuiangalia barabara hii na kuifanyia ufumbuzi ili
kuiondoa kero hii ya muda mrefu ili wakazi hao waitumie kwa amani katika
shughuli zao mbalimbali ikiwemo usafirishaji katika kujenga taifa.





0 Maoni