Muungano wa upinzani nchini Kenya
National Super Alliance (Nasa) umetoa wito kwa wafuasi wake kususia bidhaa na
huduma kutoka kwa kampuni tatu ambazo unadai zimekuwa zikimpendelea Rais Uhuru
Kenyatta.
Bw Kenyatta alitangazwa Jumatatu kuwa mshindi wa uchaguzi wa
marudio uliofanyika 26 Oktoba, ambao kiongozi wa Nasa Raila Odinga alisusia
akisema haungekuwa huru na wa haki.
Bw Odinga alitangaza kabla ya uchaguzi huo kwamba muungano huo
utabadilika na kuwa Kundi la Pingamizi dhidi ya Serikali na baadhi ya hatua
ambazo ulisema utachukua ni kususia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni ambazo
alidai zinamfaa Bw Kenyatta.
Kampuni ambazo Nasa wamesema wafuasi wao wanafaa kususia ni:
•Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, ambayo ndiyo tajiri zaidi
miongoni mwa kampuni za Kenya
•Kampuni ya maziwa ya Brookside, inayomilikiwa na familia ya
Kenyatta
•Kampuni ya kutengeneza mafuta ya kupikia na sabuni ya Bidco
Safaricom leo ilitangaza Safaricom kukua kwa faida yake baada ya
kutozwa ushuru kwa kipindi cha nusu mwaka kilichomalizika tarehe 30 Septemba
kwa asilimia 9.5 hadi Sh26.2 bilioni.
Kampuni hizo kufikia sasa hazijazungumzia hatua hiyo ya upinzani
ya kuwataka Wakenya kususia bidhaa na huduma zao.
Bw Odinga alisusia kushiriki uchaguzi huo wa mwezi uliopita
akishinikiza mageuzi yafanywe kwanza katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Uchaguzi huo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu kufuta
matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ikisema ulikuwa na kasoro nyingi.
Mahakama hiyo ilikuwa inatoa uamuzi katika kesi iliyokuwa
imewasilishwa na Bw Odinga kupinga matokeo hayo.
Bw Kenyatta alishinda uchaguzi huo wa marudio kwa kura 7.5
milioni ambazo ni sawa na asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
Idadi ya waliojitokeza ilikuwa ni asilimia 38.84 ya waliokuwa
wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo.
Matokeo kamili
ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na IEBC
Mgombea
|
Chama
|
Kura
|
Asilimia
|
Uhuru
Kenyatta
|
Jubilee
|
7,483,895
|
98.28
|
Raila
Odinga (Alisusia)
|
ODM
|
73,228
|
0.96
|
Mohamed
Abduba Dida
|
ARK
|
14,107
|
0.19
|
Japheth
Kavinga Kaluyu
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
8,261
|
0.11
|
Michael
Wainaina Mwaura
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
6,007
|
0.08
|
Joseph
Nthiga Nyagah
|
Mgombea
wa kujitegemea
|
5,554
|
0.07
|
John
Ekuru Aukot
|
Thirdway
Alliance
|
21,333
|
0.28
|
Cyrus
Jirongo
|
UDP
|
3,832
|
0.05
|
Uchaguzi ulitatizika sana katika maeneo yenye wafuasi wengi wa
upinzani. Katika majimbo manne magharibi mwa Kenya ambayo ni ngome ya Bw
Odinga, uchaguzi uliahirishwa kwa siku kadha na baadaye haukufanyika.
Nasa wameituhumu Safaricom - ambayo ilikuwa imepewa kazi ya
kupeperusha matokeo na tume ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura hadi
kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo - kwa kushiriki katika njama ya
kuchakachua matokeo.
Safaricom imekanusha tuhuma hizo.
Zaidi ya 90% ya simu zinazopigwa nchini Kenya hupigwa kupitia
mtandao wa Safaricom, ambayo ni maarufu sana kutokana na huduma ya kutuma na
kupokea pesa kwa njia ya simu, M-Pesa.


0 Maoni