NA.MWANDISHI WETU
Canada
imetangaza kuwa inamfukuza balozi wa Venezuela Wilmer Barrientos Fernández
Waziri wa
mashauri ya nchi za kigeni Chrystia Freeland alisema kuwa hatua hiyo ni jibu kwa
kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wake wa cheo juu kutoka Venezuela mwishoni mwa
wiki.
Venezuela
iliilaumu Canada kwa kuingilia masuala yake ya ndani.
Cadana ilikuwa
imeilaumu serikali ya Rais Nicholas Maduro kwa ukiuja wa haki za binadamu.
Zaidi ya watu
120 wameuawa wakati wa miezi kadha ya kuipinga serikali mapema mwaka huu.
Trump
Bi Freeland
alisema kuwa Bw. Barrientos alikuwa tayari nje ya nchi na hataruhusiwa kurudi
Cnada huku afisa mwingine wa kibalozi naye akitakiwa kuondoka.
Canada tayari
ilikuwa imewawekea vikwazo maafisa wa vyeo vya juu wa Venezuela katika hatua
ambayo iliikasirisha serikali ya Venezuela.
Venezuela pia
ilimfukuza balozi wa Brazil Ruy Pereira, kutokana na madai kuwa serikali yake
imekiuka sheria..
Marekani
ilimwekea vikwazo Maduro na utawala Trump umemtaja kuwa mtawala wa kiimla.
Upinzani umemlaumu
Bw Maduro na mtangulizi wake hayati Hugo Chavez kwa kuharibu uchumi wa nchi
kutokana na sheria zao za kisoshiolisti.
SOURCE.BBCSWAHOILI.COM


0 Maoni