NA. MWANDISHI WETU
Afisa wa cheo cha juu wa jeshi nchini
Uingereza ameonya kuwa Urusi inaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kwa
uchumi ikiwa italenga nyaya za mawasiliano ya mitandao zinazopitia chini ya
bahari.
Sir Stuart Peach, mkuu wa majeshi, alisema
kuwa nyanya hizo zinaweza kukatwa au kuharibiwa.
Madai hayo yanazua maswali kadhaa:
§
Hiki ni kitu Urusi inaweza kukifabnya?
§
Ni kitu gani kitatokea ikiwa itafanya hivyo au
ikiwa mtu mwingine atafanya hivyo?
Nyaya hizo ni za
kufanyia nini?
Zinatumiwa katika mawasiliano ya mitandao kati
ya ya nchi tofauti na mabara.
Nyaya zote hizo 428 zinachukua umbali wa
kilomita milioni 1.1 na kuzunguka dunia nzima.
Kiwango kikubwa cha data husambazwa kote
duniani nchini ya bahari kwa nyaya na zingine hjuwa nyembamba kama karatasi.
Kwa bahati mbaya, huku teknoljia yao ikiwa
inategemewa sana, nyaya hizo zinaweza kuharibiwa. Nyaya hizo hufunikwa na
plastiki, lakini nyingi bado zina upana wa sentimita tatu.
Majanga ya asili yanaweza kuziharibu na au
hata meli ikitia nanga. Hicho ndicho kilitokea katika bandari ya Alexandria
nchini Misri na kusababisha kukatwa mawasiliano kati ya Ulaya, Afrika na Asia.
Ni kwa nini wakuu ya
jeshi wana hofu?
Mwandishi wa masuala ya ulinzi wa BBC Jonathan
Beale anasema kuwa hofu ya Urusi kuweza kukata au kuharibu nyaya za chini ya
bahari inazidi kuongezeka.
Nyambizi za Urusi zinazidi kuonekana sana
bahari ya North Atlantic, hasa eneo lililo kati ya Grenland, Iceland na
Uingereza.
Marshal Peach anasema kuwa Uingereza na
washirika wake wa Nato wanakosa nyambizi, meli na ndege za kufanyia ujasusi.
Ni kitu gani kitatokea
ikiwa nyaya hizo zitakatwa?
Keir Giles ambaye ni mtaalamu wa masuala ya
vita vya mawasiliano vya Urusi, anasema kuwa hilo halina uwezekano wa kutokea
kwa sababu linaweza pia kuiathiri Urusi, lakini ni kitu ambacho pia Urusi
inaweza kukifanya.
Anasema kuwa watu hata hawatakuwa na uwezi wa
kuingia kwneye mtandao wa Facebook.
"Biashara ya kimataifa na malipo ya
mashirika ya fedha hufanywa kupitia nyaya za chini ya bahari. Madhara ya uchumi
yatakuwa ni makubwa."
Anaamini Urusi inataka kufahamu na kuacha
kutegea sana mitandao na kubuni njia zake mbadala na kutaka kufahami pia kuhusu
ni kipi kitatokea ikiwa mawasiliano ya mitandao yatavunjika.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni