NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Wakazi
waishio katika mtaa wa mazimbu rodi kata ya lukobe manispaa ya morogoro
wameendelea kupaza sauti zao wakilalamika juu ya tatizo la maji kuwa ni tatizo
la muda mrefu mpaka sasa.
Aidha
mmoja wa wakazi hao Bw. James Lyanga amesema kuwa maji katika mtaa huo yamekua
kitendawili kisicho kua na jibu kwa muda mrefu sasa pasipo kufanyiwa utatuzi.
Vilevile
Bw.Lyanga amesema maji huwa yanatoka mara moja tu kwa wiki napengine huwa
hayatoki kabisa hata kwa muda wa wiki mbili jambo ambalo huwapa tabu wakazi
hao.
Lyanga
ameonesha kushangaa kuona maji yakiuzwa kwa kutumia magari[boza] pamoja na
pikipiki za magurudumu matatu vibajaji]
“Ndugu mwandishi nashangaa kuona maji yakiuzwa kwa kutumia maboza pamoja
na vibajaji huku nikishindwa kuelewa wao maji hayo wanayatoa wapi? Na kama wao
wanayapata maana yake wahusika wameona kuwa wakiwauzia hao ndipo wanapata faida
kuliko kutumia mabomba yaliyopo mtaani? Hayo ni maswali ambayo ndugu mwandishi
wakazi tunakosa majibu” mwisho wa kunuku.
Lyanga
amemaliza kwa kusema kuwa imekua tabia pale wananchi wanapo andamana huwa maji
yanatoka na baada ya muda kidogo yanakua hayatoki tena.
Pia
Bi.Edith Mushi amesema kutokana na shida hiyo ya maji wanalazimika kununua maji
kutoka kwenye magari yanayo uza maji ambayo huuzwa kwa bei kubwa kati ya Tsh.
300- 500 kwa ndoo moja kubwa.
Bi.
Edith ameongeza kusema kutokana na hali ngumu iliyopo kwa sasa wanashindwa
kununua maji mengi hivyo baadhi ya shughuli zinazo hitaji maji mengi kama kufua
nguo kukwama.
Wakazi
hao wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwasababu limekua kero na
mateso kwa wakazi hao na likiwa ni
tatizo tokea muda mrefu.
Miezi
mitatu iliyopita kituo cha plan media tulichapisha habari juu ya suala hili
lakini bado kero hii haijafanyiwa ufumbuzi mpaka leo hii.


0 Maoni