NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Wakazi
wa eneo la uwanja wa ndege [airport] manspaa ya kigoma ujiji wamepaza sauti zao
wakilalamikia tabu ya maji inayo wakumba
wakazi hao kwa muda mrefu mpaka leo hii.
Aidha
Bi. Mwajuma Ally Mwinyi amesema mtaa huo umegubikwa na kero ya maji jambo
ambalo huwalazimu kutumia maji ya visima wanavyo chimba ili kupata maji kwa
matumizi ya majumbani.
Bi.Mwajuma
ameongeza kwa kusema kuwa maji hayo si salama kwa matumizi ya majumbani hasa
kwa matumizi ya kunywa kwani wanaweza kupata ugonjwa wa mripuko kama kichocho
na kipindupindu.
Kwa
upande wake Bw.Fred Hamenya kumesema kuwa waliahidiwa kuwa mapema mwezi huu
mradi huu unge kamilika lakini mpaka leo hii hakuna dalili zozote za kupata
maji safi na salama.
Pia
Hamenya amemaliza kwa kusema kuwa kwa sasa wanaishukuru mvua inapo nyesha
wanapata maji ya kunywa lakini katika kipindi cha kiangazi hulazimika kutumia
maji ya kisima.
Vilevile
wakazi hao wameiomba serikali kushughulikia tatizo hilo katika mwaka ujao wa
2018 ili kunusuru afya na maisha ya wakazi hao katika kulijenga taifa imara
lisilo na maradhi.


0 Maoni