NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Mvua zinazo endelea kiunyesha katika kijiji cha isubangala na kata ya
ilangu kwa ujumla wilaya ya katavi vijijini
imefanya uharibifu mkubwa wa mazao ikiwemo mahindi,maharage pamoja na
tumbaku kutoka na mvua nyingi zinazo nyesha kila siku.
Aidha Bw.Living Sharutiel ni mkazi wa kijiji cha
isubangala ameieleza plan media kuwa mvua hiyo imeleta madhara makubwa kiasi
kwamba mazao yameharibiwa hususa ni maharage, mahindi pamoja na tumbaku.
Hata hivyo living ameieleza plan media kuwa kwa watu
ambao waliweka mbolea kwenye mazao siku za hivi karibuni nisawa na kazi bure
kutokana na mbolea hiyo kusombwa na maji.
Kwaupande wake Bi. Sifa Bartazal amesema kuwa mvua
hizo zinazo endelea zinafanya shuguli nyingi kusimama huku wakishindwa kwenda
shambani kutokana na mvua hizo kunyesha kila wakati.
Pia Bi. Brtazal ameongeza kwa kusema kuwa mito imefurika maji jambo ambalo linawafanya
washindwe kuvuka kuelekea sehemu mbalimbali kwasababu mito hiyo ina madaraja ya
kienyeji ambayo walitumia miti kutengeneza hivyo kujaa kwa mito hiyo
imesababisha madaraja hayo kusombwa na maji.
Bi. Bartazal amamaliza kwa kusema kuwa kwa wale
wakulima wa tumbuku nyumba za kukaushia tumbaku [BANI] zinabomoka kila kukicha
na ni hasara kubwa kwa wakulima hao kwasababu msimu wa kukausha tumbaku
unakaribia.


0 Maoni