Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

MIMBA ZA UTOTONI

NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
Kulingana na sheria za nchi yetu ya Tanzania ni kwamba mtoto ni Yule mwenye umri chini ya miaka 18 yani kuanzia miaka 17 kushuka mpaka mwaka 0 hapa ndipo tunapata maana ya neono mtoto.

Miezi kadhaa iliyopita Rais mtukufu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alitangaza kuwa katika serikali yake mwanafunzi atakae pata ujauzito hato ruhusiwa kurudi shuleni tena na huku sheria ikisema kuwa mwanaume atakae mpa njauzito mwanafunzi basi atafungwa miaka isiyo pungua 30.

Na tunapo zungumzia neono mimba ni kiumbe ambacho bado kipo ndani ya tumbo ambacho kinatarajiwa kuwa mtoto baada ya miezi tisa kutimia.

Basi mpenzi msomaji wa makala hii nikukaribishe mojakwamoja katika makala hii ya leo ambayo utapata kujifunza mengi na ambayo ulikua hujui na kama ulikuaunajua basi tunakuongezea maarifa zaidi.

Tunapo zungumzia mimba za utotoni ni zile mimba ambazo wanazipata watu ambao wako chini ya miaka 18 na hii moja kwa moja zinakua ni mimba za utotoni.

Aidha mimba za utotoni ni mimba ambazo zinapatikana kimakosa kwasababu haziruhusiwi kisheria kwa mtu mwenye umri huo kuubeba ujauzito.

Sheria ya nchi yetu ya Tanzania inapiga vita dhidi ya mimba za utotoni na huku bado baadhi ya watu na hasa vijijini wamekua wakivunja sheria hii aidha kwa kujua ama kwa kuto kujua juu ya suala hilo.

Kwa mjibu wa sheria za nchi mwanamke anatakiwa ama anshauriwa kubeba ujauzito akiwa a na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea na hasa akiwa amesha olewa.

Nilibahatika kufanya mahojiano na Aisha Athumani binti wa kizaramo aishie jijini Dar es salaam ambae hakupenda kuchukuliwa picha yake wala mahali anapo ishi na wala shule aliyokua akisoma alikua na haya ya kusema “Kwa majina naitwa Aisha Athumani naishi Dar es salaam nina miaka 16 nimeishia kidato cha kwanza baada ya kupewa ujauzito na mwanaume alie nipa ujauzito aliamua kukimbia na mpaka leo hii hajulikani alipo istoshe kwasasa siwezi tena maana nimesha kua mzazi na mtoto huyu unae muona ni mwanangu nalea kwa sasa,baada ya kupata ujauzito huu nilifukuzwa shule na wazazi wakanifukuza nyumbani wakasema nisipokuja na alie nipa ujauzito huo nisikanyage nyumbani kwao na hivi unavyo niona naishi kwa neema ya Mungu na mwanangu huyu unae muona ndugu mwandishi” mwisho wa kunukuu.

Hatahivyo Aisha hakuishia hapo aliongeza kwa kusema kuwa kilicho mponza na kupata ujauzito huo kuwa ni tama zake mwenyewe kwasababu alilelewa katika malezi mazuri, malezi ya dini hivyo anajutia kosa hilo linalo mfanya kuishi maisha magumu kwa sasa.

Pia aisha alitoa ushauri kwa watoto wa kike kuto kujihusisha na mahusiano ya kingono kingali wadogo kwakua madhara yake ni makubwa na badala yake wajihusishe na elimu na si vinginevyo.

Binti Aisha ni moja kati ya mabinti wa kitanzania ambae amekutana na suala hilo lakini tunapaswa kujifunza kupita yeye ili kuondokana na tatizo hilo la mimba za utotoni.

Vilevile kuna visababishi vya mimba hizi kupatikana na ni vingi sana lakini siku ya leo tutapata kuzungumzia machache kati ya hauyo mengi yasababishayo mimba hizo za utotoni.

Mila na tamaduni, sitaki kusema kuwa mila ndizo husababisha mimba hizo hapa ukweli nikwamba mila nazo huchangia hili kwasababu baadhi ya mila na tabaduni za kitanzania na hasa jamii za wafugaji huwa zinaruhusu mabinti zao kuolewa wakiwa na umri mdogo nahii ikiwa ni ukosefu wa elimu.

Tamaa, Ninapo zungumzia tama unzweza usinielewe vizuri lakini maana yangu nikwamba unakuta binti kulingana na hali ngumu ya kimaisha iliyopo nyumbani kwao anatamani kupata kitu fuani anajikuta akijiingiza katika kufanya ngono akiwa na umri mdogo ili kupata kile anacho kihitaji na hatamae anajikuta akipata ujauzito pasipo kutarajia.

Makundi rika,Binti anapokua katika hatua za ukuaji huwa anapata marafiki wema na wabaya wa rika lake na anapo pata marafiki wabaya basi anajikuta akishawishiwa na kujiiingiza kwenye mahusiano ya kingono akiwa na umri mdogo na hatimae kupata ujauzizo.

Utandawazi, ujio wa  sayansi na teknolojia katika karna hii ya 21 ime athiri sana maisha ya asili na kila mtu anaitumia teknolojia atakavyo hususa ni matumizi ya simu kwa kiasi kikubwa simu zinatumika sana katika mawasikiano hivyo ikitumika vibaya huwa mawasiliano hayo huwasababishia watoto hao kupata ujauzito.

Uhuru kupita kiasi, binti anapo pewa uhuru wa kupita kiasi basi binti hujisahau na kujiingiza katika mahusiano ya kingono nahii hupelekea binti huyo kubeba ujauzito katika umri huo.

Basi mpenzi msomaji wa makala hii hayo yalikua ni baadhi ya mengi yanayo sababisha mimba za utotoni  na umeweza kujionea ni jinsi gani zinapatikana mimba hizo.

Vilevile kuna madhara yatokanayo na mimba za utotoni hivyo  leo hii tutaenda kuzungumzia machache kati ya mengi ambayo huwapata watoto wa kike wanapo beba ujauzito katika umri huo.

Kuharibu ndoto, mtoto wakike anapo pata ujauzito ndoto zake za maisha yake zinakua zimeishia hapo kwasababu anakua hana nguvu na uwezo wa kufikiria maisha zaidi atafikiria kumlea mtoto wake.

Vifo, binti anapo pata ujauzito akiwa chini ya umri wa miaka 18 viungo vyake vinakua havijakomaa hivyo muda mwingine hupelekea mtoto huyo kujifungua kwa njia ya upasuaji napengine hupelekea kifo cha mama na mtoto.

Maradhi, kumbuka kuwa binti huyu ni mdogo na viungo vyake havija komaa na anapo jifungua mtoto via vya uzazi vinaweza kuchanika na kusababisha maradhi kama fistula na mengineyo kama hayo.

Basi msomaji wangu hayo ni baadhi ya mengi yanayo weza kumkumba mtoto wa kike pale anapo beba ujauzito akiwa na umri mdogo maarufu kama mimba za utotoni.

Aidha jamii inahitaji elimu ya kutosha juu ya mimba za utotoni ili kuokoa kizazi hiki dhidi ya mimba za utotoni na kumuokoa mtoto wa kike wa Tanzania.

Vilevile wazazi wanatakiwa kuwapatia malezi bora watoto wao kingali watoto ili wasiweze kujiingiza katka vishawishi vya namna hii ambavyo ni vibaya kwa watoto wetu.

Pia ningependa kuishauri jamii ya kitanzania kwa ujumla kutoa elimu kwa watu ambao bado wana mila hizo potofu lengo ikiwa ni kutokomeza suala la mimba za utoni.

Tanzania bira mimba za utotoni inawezekana tuungane kwa pamoja kupambana na suala hili au mila potofu zilizo pitwa na wakati kwapamoja tukisimama twaweza.

Na huu ndio mwisho wa makala yetu kwa leo nikushukuru kwa kuchukua muda wako kusoma makala hii naamini kuna kitu umejifunza na kama ulikua unajua basi umeongeza maarifa naamini utakua barozi wa kupinga suala hili la mimba za utotoni.

USIKOSE MAKALA IJAYO INAYO HUSU NDOA ZA UTOTONI
Ø     Maana
Ø     Chanzo
Ø     Madhara
Ø     Suruhisho
Ø     Ushauri


KWA TUKIO AU TANGAZO LOLOTE TUPIGIE KWA NAMBA 0713 305 650

Chapisha Maoni

0 Maoni