uma ya viongozi wa ligi Manchester City
Mkufunzi wa Chelsea
Antonio Conte ametaja ukosefu wa bahati katika kikosi chake kama sababu
ya wao kuwa pointi 13 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester City baada
ya ushindi mzuri dhidi ya klabu ya Brighton.
Kikosi hicho cha
Conte kilirekodi ushindi wa sita mfululizo nyumbani baada ya kuonyesha
mchezo mzuri ulioimarika katika kipindi cha pili dhidi ya Seagulls huku
Alvaro Morata na Marcos Alonzo wakifunga mabao muhimu.Lakini mabingwa hao wa ligi ya Uingereza wanasalia katika nafasi ya tatu huku City wakijiandaa kukabiliana na Newcastle siku ya Jumatano.
''Msimu huu uko tofauti na msimu uliopita'', alisema Conte baada ya mechi hyo iliochezwa siku ya siku kuu ya Boxing Day.
''Msimu uliopita mara nyingi tulishinda mechi na tulikuwa na bahati, kama vile dhidi ya West Brom hapa na Sunderland. Msimu huu mara nyengine tungekuwa na bahati zaidi''.
''Tunaiheshimu sana Manchester City kwa sababu wanafanya kitu kisichokuwa cha kawaida''.
Lakini Brighton walipatikana wamezubaa kunako sekundi ya 52 ya kipindi cha pili wakati Morata alipowachenga mabeki na kufunga krosi ya Cesar Azpilicueta's kupitia kichwa.
Bao hilo lilibadilisha mambo na kuimarisha shinikizo ya timu hiyo ya nyumbani ambayo ilimtumia Eden Hazard katika jaribio la kuvunja ulinzi uliowekwa na wageni hao.
Lakini ilikuwa Alonzo aliyefunga udhia kupitia kichwa muda mfupi baada ya kukosa mabao mawili kutokana na mpira wa adhabu na kichwa.
''Katika kipindi cha pili ,tuliimarika na kutengeza nafasi nyingi'', aliongezea Conte.
''Ulikuwa mchezo mzu

0 Maoni