
Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 29, yuko namba moja katika orodha ya Barcelona lakini mabingwa hao wa La Liga wanataka kuwasaini wachezaji watano mwezi Junuari. (Marca via Daily Express)
Southampton hatimaye wamekiri kushindwa kumweka beki Virgin Van Dijk, 26, lakini hawatamuuza chini ya pauni milioni 70. (Sun)
Meneja wa Everton Sam Allardyce aamini kuwa mshambuliji wa Arsenal's Olivier Giroud atahamia Goodison Park mwezi Junuari.(Liverpool Echo)
Arsenal wako tayari kumpa mkataba wa muda mrefu kiungo wao wa kati Jack Wilshere 25. (Sun)

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku Real Mdrid wakimmezea mate nchezaji huyo wa miaka 24. (Calciomercato, kupitia Daily Express)
West Ham wanammezea mate kiungowa kati wa Sevilla Steven N'Zonzi, 29, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Everton. (Sun)


0 Maoni