NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Ukosefu
wa mwenyekiti wa kijiji kwa muda mrefu katika kijiji cha Katete kata ya
Mwakizega wilaya ya uvinza mkoani Kigoma umesababisha kukwama kwa ujenzi wa
shule uliokuwa ukiendelea katika kijiji hicho.
Aidha
Bw.Amir Juma ni mkazi wa kijiji cha katete amesema kuwa kijiji hicho hakina
mwenyekiti na badala yake kijiji hicho kinaongozwa na kaimu mwenyekiti ambae
wanaichi hao hawamtambui.
Vilevile
Bw.Juma ameongeza kwa kusema kuwa ukosefu wa kiongozi huyo imepelekea kurudisha
maendeleo ya kijiji hicho ikiwemo ujenzi wa shule uliokua ukiendele kijijini
hapo.
Kwaupande
wake Bw. Mtafiti Mikidadi ambae pia ni mkazi wa katete “B” asema kuwa uongozi wa kijiji hicho wanasema
wanalifanyia kazi lakini mpaka leo hii hivyo serikali waliangalie suala hili
kwa umakini kwani suala hilo linarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho.
Pia
diwani wa kata ya Mwakizega Mh.Swabilu Mussa Basenga amekiri kuwepo kwa tatizo
hilo na ameshalifikisha kwa mkurugenzi
na wanalifanyia utaratibu kuhakikisha wanaanda bajeti ya kufanyia uchaguzi
mdogo wa mwenyekiti wa kijiji hicho.


0 Maoni