NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Kuekea
mwaka mpya muimbaji wa nyimbo za injili
Tanzania anae fanya vizuri kwasasa Baisa
Mhela amekua akiachia video harakaharaka ambapo leo hii ameachia video
ya funga mwaka uitwao CHINI YA MSALABA kupitia cha nnel yake ya YouTube @BAISA
MHELA, Link yake bofya
hapa>>>> https://youtu.be/vFrMOX3TOblna hii ikiwa ni video ya
mwisho ndani ya mwaka huu 2017.
Baisa
amesema kuwa sababu za kuachia video harakaharaka sana kwasasa ni kuwapa Baraka
mashabiki wake na muziki wa injili kwa ujumla ili kuukaribisha mwaka mpya na
mambo mapya.
Aidha
baisa amewashukuru mashabiki zake kwa kuutambua mchango wake katika muziki wa
injili kwani ndani ya mwaka 2017
amefanikiwa kukamilisha albam ya DVD yenye nyimbo takribani 7 pamoja na kuingia
mkataba na kampuni za mukiziki Tanzania na Kenya kuweka muito kwenye simu
[ringtone], lakini pia alifanikiwa kufanya huduma kwenye mikutano na matamasha
mbalimbali.
Vilevile
Baisa alipitia changamoto mbalimbali ikiwemo kampuni aliyo kua akifanya nayo kazi mwaka huu kuchelewesha kazi zake ili
ziwafikie walengwa lakini pia kurudiarudia baadhi ya kazi kutokana na kazi hizo
kukosa ubora.
Pia
Baisa amesema hatoweza kuzindua albam ya DVD na badala yake ameamua kutoa video
ya wimbo mmojammoja lengo ikiwa ni kuwabariki mashabiki zake pamoja na kuwaanda
kupokea kazi nzuri zijazo hapo mwakani pia amewaomba mashabiki kununua nyimbo
zake kupitia wasambazaji wake.
Hata
hivyo Baisa amemalizia kwa kusema kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya
uitwao JUST mapema mwakani hivyo
amewaomba mashabiki zake kukaa mkao wa kula kuupokea wimbo huo mpya na wenye
ubora wa hali ya juu.
WASILIANA NA BAISA MHELA KUPITIA NAMBA 0652 155 399


0 Maoni