NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Wakazi
wa kijiji cha Katete kata ya Mwakizenga wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
wamelalamikia uongozi wa kijiji kwa kuzorotesha
ujenzi wa zahanati unaoendelea katika kijiji hicho huku wakiendelea kupata adha
ya vifo kutokana na kutembea umbali wa zaidi ya saa moja kukifuata kituo cha
afya cha Mwakizega ili kupata huduma hiyo.
Aidha Bw.Amri Ibrahim ni mkazi wa kijiji hicho
amesema kuwa wanapata tabu sana kuwasafirisha wagonjwa mahututi hususani wamama
wajawazito umbali wa kilometa 9 kwa kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki
kukifuata kilipo kituo cha afya cha mwakizega.
Kwaupande
wake Bw. Mtafiti Mikidadi Amesema kuwa wamekuwa wakichangishwa michango
mbalimbali ilikuwezesha ujenzi wa zahanati hiyo lakini mpaka leo hii hakuna
mafanikio ya kuendeleza ujenzi wa zahanati hiyo.
Vilevile
diwani wa kata ya Mwakizega Bw.Swabiru Basenga amekiri kuwepo kwa tatizo hilo
na hivyo aliamua kufanya mkutano wa hadhara na kuchangia mifuko 30 ya seruji
lengo ikiwa ni kuhamasisha wananchi wengine kuchangia ujenzi huo.
Hata
hivyo Basenga amemalizia kwa kusema kuwa
alilazimika kuteua nyumba kijijini hapo ambayo inatumika badala ya zahanati
pamoja na kuchagua timu ya wataalamu ambayo hufika kijijini hapo mala mbili kwa
kila wiki wakati wakisubiria ujenzi huo ukamilike.
Pia
wakazi hao wameiomba serikali kuliangalia suala hilo ili kuokoa uhai wa wakazi
hao pamoja na maendeleo ya kijiji hicho kwani sera ya nchi inasema kila kijiji
kinatakiwa kiwe na zahanati lakini kijiji hicho bado hakijapata zahanati.


0 Maoni