NA. GOODLUCK CHRISTOPHER
Mshambuliaji machachari wa timu ya Liverpool ambaye ni raia wa
Misri, Mohamed Salah ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa
mwaka 2017 na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Salah alikuwa
akishindana na Pierre-Emerick Aubameyang, na Sadio Mane na akaibuka bora zaidi
kwa wingi wa kura na ubora awapo kiwanjani.
Mane na Salah
walihudhuria sherehe za kutangazwa kwa washindi mjini Accra, Ghana saa 24 kabla
ya mechi ya Kombe la FA Ijumaa ambapo klabu yao ya Liverpool itacheza dhidi ya
Everton.
Salah alionekana
kuitetea vyema timu yake ya Liverpool mwaka 2017 baada ya kujipatia goli 23
katika mechi 29 baada ya kujiunga katika ligi kuu ya England akitokea timu ya
AS Roma.
Wapinzani wake nao si
haba kwani Pierre-Emerick Aubameyang, wakati huo huo, alifunga mabao 31 ya
kipekee kati ya michezo 32 katika mashindano yote ya mwisho.
Tuzo hiyo ya
shirikisho la soka barani Afrika ilikuwa na orodha ya wachezaji wapatao 24,
lakini mwezi Desemba Salah, Aubameyang na Mane walitangazwa kuingia katika
hatua ya mwisho ya tatu bora .
Mshindi wa tuzo hiyo
kwa mwaka uliopita alichaguliwa na makocha kwa kushirikiana na manahodha wa
timu katika kila timu ya wanaume ya taifa barani Afrika.
Mwenzake Sadio Mane
kutoka katika timu ya Liverpool Sane alikuwa mshindi wa pili kwa wingi wa kura,
naye nyota mchezaji wa timu ya Dortmund, Aubameyang akaushika nafasi ya tatu
kwa wingi wa kura.
Wengine waliopata tuzo
hiyo ni Mwanasoka bora wa kike wa Afrika Asisat Oshoala (kutoka Nigeria)
Mwanasoka bora kijana
Patson Daka (kutoka Zambia & Liefering)
Kocha bora wa mwka ni
Hector Cuper (Misri)
Klabu bora ya mwaka ni
(Wydad Athletic Club )
Timu bora ya Taifa yam
mwaka ( Misri)
Timu bora ya taifa ya wanawake
ni (Afrika Kusini)
Legend Ibrahim Sunday
(Ghana)


0 Maoni