Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

KUFUTI KWA ZEBRA YA HATARISHA MAISHA YA WATU KIGOMA.

NA.GOODLUCK CHRISTOPHER.
Wananchi  wa  Katubuka manispaa ya kigoma ujiji wameilalamikia serikali kufuatia kufutika kwa alama za kivuko vya watembea kwa miguu katika barabara ya uwanja wa ndege hali inayo pelekea kutokea  kwa ajari pindi wanapo vuka barabara.

Maurid Ally ni mmoja kati ya wakazi wa mwanga ambae amesema kuwa kufutika kwa vivuko hivyo ina sababisha kutokea kwa ajari kutokana na madereva wa vyombo vya moto kama Magari,Bajaji na Pikipiki kupita kwa kasi pasipo kuzingatia uwepo wa alama hizo.

Aidha Ally amesema kwamba katika mwaka uliopita alishuhudia mtoto mmoja akigongwa na gari huku wengine wakijeruhiiwa mara kwa mara hususa ni wanafunzi washule ya msingi ya Katubuka pamoja na Mwenge.

Kwa upande wake Ashel Kaguta ambae pia ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa hili ni tatizo kubwa hususa ni nyakati za usiku ambapo madereva hutembea kasi huku wengine wakiwa ni wageni wa njia hiyo.

Vilevile Kaguta amemaliza kwa kusema kuwa serikali wanapaswa kuliangalia tatizo hili kwa jicho lapili ili kunusuru wakazi waeneo hilo hususa ni watoto washule.

Sikuishia hapo nikaumua kumtafuta meneja wa TARURA  Manispaa ya kigoma ujiji Bw. Issa Ally Ryanga ambae amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kuwa wanapanga bajeti kwa ajiri ya kuweka alama hizo haraka iwezekanavyo.
Pia Ryanga amemaliza kwa kusema kuwa si kufutika kwa alama hizo tu bali wanatarajia kufukia mashimo pamoja na kurudishia alama zote za barabarani [road singn] kwasababu havihitaji pesa nyingi kurekebisha.

Ikumbukwe kuwa barabara hii ni moja kati ya barabara ambazo zimefutika alama hizo katika manispaa ya kigoma ujiji yingine ikiwa ni barabara ya Noradi ,Kibirizi n.k


Chapisha Maoni

0 Maoni