NA.MWANDISHI
WETU
Mshindi wa tuzo ya Academy Lupita Nyong'o,
atachapisha kitabu chake cha kwanza kuhusu watoto ''Sulwe'' akishirikiana na
wachapishaji wa vitabu vya Simon na Schuster kwa wasomaji wadogo Januari.
Sulwe ikimaanisha
'nyota' kwa lugha ya Kiluo ni hadithi ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
mitano ambaye amelelewa nchini kenya.
Katika kitabu hicho ,
Sulwe ni msichana mweusi katika familia yake, swala linalomfanya kuwa na
wasiwasi na sasa ameamua kutafuta njia ya kung'arisha ngozi yake na kuwa
mweupe.
Huku habari hiyo
ikiendelea, Sulwe anaanza safari ambayo kupitia ushauri wa mamake inamsaidia
kuelewa urembo kwa njia tofauti.
Kwa Bi Nyongo, uamuzi
wa kugusa ama kuzungumzia kuhusu mada hii nzito katika kitabu cha watoto
ulikuwa wazi.
Hadithi hiyo inapanda
mbegu katika akili ya wototo , hatua inayoruhusu watoto kupata mafunzo ambayo
hawayatambui wakati wanaposoma vitabu, alisema bi Nyongo katika mahojiano.
Wakati anapofikiria
kuhusu safari yake ya kuikubali nafsi yake na kujipenda, bi Nyong'o anasema
kuwa hatua yake ya kusoma na mamake ilimsaidia sana katika ukuwaji wake.
Kama Sulwe, Bi Nyongo
aliyeigiza katika filamu za "Star Wars: The Force Awakens alijitahidi na
rangi yake katika utoto wake.Alikumbuka kujitambua katika shule ya upili na
kujali kuhusu maono ya watu wengine.
Ni wakati huo ambapo
aligundua lugha inayotumiwa na watu wa nje ya familia yake kuelezea rangi ya
ngozi ya dadake waliodai kuwa ''nzuri''.
Bi Nyongo alitambua
kuwa na wasiwasi kuhusu ngozi yake katika hotuba isioweza kusameheka 2014.
Baadaye alitumia tamko
lake kuwasilisha ujumbe mkali kuhusu umuhimu wa rangi na uwakilishaji katika
Hollywood na kwengineko.
Pia alizungumza na
shabiki wake kijana ambaye aliamua kutojichubua ili kuwa na rangi ya kung'ara
baada ya kushuhudia ufanisi wa Bi Nyongo kama mwigizaji.
SOURCE. BBCSWAHIL.COM


0 Maoni