NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Ni takribani mwezi mmoja tangu vyoo vya kituo cha
daladala cha ujiji katika manispaa ya kigoma ujiji kujaa na kutelekezwa jambo
linalo hatarisha maisha ya madereva pamoja na abiria wanao tumia kituo hicho.
TUNAOMBA RADHI KWA MUONEKANO WA PICHA HII HAPO JUU.
Plan Media ilipata kufika katika kituo hicho
kujionea haliharisi pamoja na kuzungumza na baadhi ya madereva lakini pia
abiria ambao wameitupia lawama chama cha wamiliki wa Daladala mkoa wa Kigoma
KIBOA kwa kushindwa kurekebisha miundombinu ya vyoo hivyo.
Aidha Samwel Gabliel ni mmoja wa madereva ambae
amesema kuwa wamekua wakilipia shilingi 1000 kwa kila siku lakini wakiingia
katika vyo hivyo wanashindwa kujisaidia kutokana na kujaa pasipo kufanyiwa
usafi.
Kwa upande wake Mrisho Mashaka amesema kuwa imefikia
hatua wanalazimika kutumia vyoo vya nyumba zinazo patikana karibu na kituo hicho jambo ambalo ni usumbufu kwao
ikilinganishwa na kipidi hiki cha masika ambapo ni rahisi kupatwa na magonjwa
ya mlipuko.
Vilevile Addul Juma ni mmoja wa abiria anae toka
Ujiji kuelekea Kibirizi kuwa haoni haja ya kupandia gari ndani ya kituo hicho
kwasababu kituo hicho hakina manufaa kwa watumiaji na badala yake anaamua
kusubiria gari nje ya kituo hicho.
Hata hivyo watumiaji wa kituo hicho wameuomba uongozi
wa wamiliki wa daladala kwa mkoa wa Kigoma KIBOA kurekebisha miundo mbinu ya
vyoo hivyo ili kuwanusuru na afya zao kutokana na magonjwa ya mripuko yanayo
weza kujitokeza.
Plan Media haikuishia hapo ikaamua kumtafuta
Mwenyekiti wa KIBOA BW. Ibrahim Zubari
ili kujua mwafaka wa tatizo hili ambae ameonesha kuto kujua tatizo hili na
kuahidi kwamba analifanyia mchakato ili liweze kutatuliwa.
Vilevile Zuberi amekana kupokea kiasi cha Sh.1000 na
kufafanua kuwa pesa hiyo ni tozo ya manispaa ambayo madereva hao wanapaswa
kutozwa katika vituo vyote vya daladala ndani ya manispaa ya kigoma ujiji.
Ikumbukwe kuwa mkoa wa kigoma ni moja kati ya mikoa
ambao umekua ukikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu hususa ni ukanda wa ziwa
Tanganyika na chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wasio na utu kujisaidia pembezoni
mwa ziwa hilo, hivyo basi hatua zinapaswa kuchukuliwa haraka iwezekanavyo ili
kujiepusha na madhara makubwa yanayo weza kujitokeza katika kituo hicho.



0 Maoni