NA.GOODLUCK
CHRISTOPHR
Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa hakuna kitu
kinaitwa UKAWA kwani mpango huo ulianzishwa na CHADEMA ili kuvitumia vyama
vingine kisiasa.
Polepole amesema kuwa
kama UKAWA ingelikuwepo hadi leo basi isingetokea baadhi ya majimbo CHADEMA
kushindana na CUF ile hali vyama vyote vipo chini ya muavuli wa UKAWA.
“Hakuna kitu kinaitwa
UKAWA, hii ilikuwa project ya Chadema ikivitumia vyama vingine, CUF, NCCR na
NLD. Kilichobaki ni UKIWA, katika jimbo lililokuwa la CUF leo CDM na CUF
wanamenyana,”ameandika Humphrey Polepole kupitia Twitter.
Hata hivyo, kwenye
uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni CUF kwa upande wa Prof
Lipumba imesimamisha mgombea wake huku CHADEMA nao wakisimamisha mgombea wao.


0 Maoni