Na. goodluck christopher
Elimu
ni kitu cha msingi sana katika maisha ya binadamu na vitabu vya Mungu pia
vinasisitiza elimu kuwa ni jambo la kuzingatia sana maana katika karne hii ya
21 suala la elimu limekua ni lamsingi na la maana sana ikizingatiwa kuwa
asilimia kubwa za vitu vina hitaji elimu hivyo suala hili halikwepeki kwa mtu
yeyote.
Katika
miaka kadhaa iliyo pita elimu ilikua haizingatiwi kwa kiasi kikubwa hususani
vijijini na hasa kwa watoto wakike ambapo iliaminika kuwa watoto wakike ni
wakubaki nyumbani huku wakisubiraa kuolewa jambo ambalo lilikua ni imani potofu
na ukoefu wa elimu.
Mbali
na elimu kutolewa juu ya hilo bado kuna jamii zinaendelea na imani hizo potofu
ambazo zimepitwa na wakati huku jamii hizo zikiwa zinaamini kuwa ni sahihi
kufanya hivyo na hasa katika maeneo ya vijijini.
Mpenzi
msomaji wa Plan Media napenda kuku karibisha rasimi katika makala hii yenye
mafundisho ya hali ya juu kuhusiana na wafanya kazi wa majumbani kwamaana ya wadada
wanaofanya kazi za ndani [HOUSE GIRL].
Tunapo
zungumzia wafanya kazi wa ndani ni watu/mtu ambae ameajiriwa kwaajili ya
kusaidia ama kufanya kazi za nyumbani ili kujipatia kipato cha kujiendeshea
maisha yake kama zilivyo kazi zingine ambazo watu huzifanya kwa ajili ya
kujiendeshea maisha ya kila siku.
Kama
mfanya kazi mwingine alivyo kua na haki
basi hata mfanya kazi wa ndani anahaki vilevile ambazo anahitaji
kuzipata anapo kua akifanya kazi yake hiyo ili aweze kufaidika na kazi hiyo.
Tanzania
na dunia nzima kwa ujumla inapiga vita dhidi ya ajira kwa watoto kwa maana
yakuwa mtu akiwa chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kuajiriwa bali anatakiwa
apate haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Mbali
na dunia nzima kupinga suala hili katika nchi yetu ya Tanzania bado asilimia
kubwa ya wafanya kazi wa ndani wako chini ya umri wa miaka 18 jambo ambalo ni
kosa kisheria kwa kuwaajiri watoto hao.
Aidha
wafanya kazi wa ndani ni watu ambao kwa asilimia kubwa huwa hawatendewi haki
kwasababu huwa wanafanya kazi kubwa huku
wakilipwa ujira mdogo sana ukilinganisha na kazi wanazo zifanya.
Vilevile
hakuna mikataba inayo walinda wafanyakazi hawa hivyo muajiri huwa anampangia
vile anavyo jisikia na muajiriwa huyo hulazimika kufuata kile anacho pangiwa na
muajiri wake.
Kipigo,
matusi na udharirishaji huwakumba wadada hawa kutokana na umri wao na hata wanapo jitetea bado waajiri wao
wanakua siyo waelewa maana wao hutumia nguvu na mamlaka waliyo nayo katika nyumba
yani baba au mama na wakati mwingine watoto wa nyumba hiyo.
Kilio
na machozi yawa wafanya kazi wa ndani huishia kwenye geti la chuma na ukuta
mrefu pamoja na nyumba yenye milango iliyo fungwa na madirisha yenye vioo
vyeusi kama gari za kubebea watu maarufu pasipo kupata msaada wowote na muda
mwingine huwekewa walinzi.
Pia
asilimia kubwa ya wafanya kazi hawa hutolewa maeneo ya vijijini, watoto hawa
huwaraghai kuwa wataishi maisha mazuri,maripo mazuri na hata huahidiwa
kupelekwa shuleni jambo ambalo huwavutia waoto hao kufanya kazi hizo.
Nyuso
za watoto hao hutabasamu pale wanapo fika mjini na kuona mataa kama waswahili
wanavyo sema, jumba lenye geti,ukuta na madirisha ya vioo na ndani kukuwa na
masofa ya kisasa, Runinga ya
kisasa,kipuliza upepo na vingine vizuri kama hivyo ambavya havipatikani maeneo
ya vijijini.
Mabinti
hawa nyuso zao hutanda giza na kukunjamana kama wazee wenye miaka 90 huku
wakiwa na miaka kati ya 12-17 kutokana na kipigo pamoja na manyanyaso wanayo
yapata ya kila siku wawapo katika majumba hayo ya kifahari.
Kutokana
na umri wao wanashindwa kuchukua maamzi yaliyo sahahi kwao kama kutoa taarifa
kwa majirani, viongozi wa serikali ama wazazi wao kutokana na vitishowanavyo
pewa.na waajiri wao.
Wakati
nikitokea Dar es salaam kueleke mkoa wa Kigoma kwa kutumia usafiri wa treni
nilikutana na binti mwenye umri wa miaka 15 ambae hakupenda jina lake litajwe,
Binti huyu ni mzaliwa wa Tabora wila ya urambo nilibahatika kukaa karibu nae na
katika mangumzo yetu nilimuona kama binti mdogo lakini anasafiri akiwa peke
yake nikaamua kufanya nae mahojiano.
Katika
mahojiano na binti huyo, binti alikua na
haya ya kusema, “Nina miaka 15 ni mzaliwa wa Tabora
wilata ya urambo na hivi unavoniona nimetokea mkoani Morogoro, nina miaka
mitatu nikiwa nipo mkoani morogoro na nimekua nikifanya kazi za ndani. Kusema
ukweli nimekua nikifanya kazi hii tangia nikiwa na miaka 13 lakini sijaona
mafanikio yake kwa maana nimekua nikipokea manyanyaso makubwa, kipigo na matusi
kutoka kwa waajiri wangu huku nikipewa ujira mdogo kiasi cha Tsh.15000 kwa
mwezi na pesa hiyo nakuwa sipewi kwa wakati, niliyazoea maisha hayo japo
nilikua siyapendi ndipo nilibahatika kutoroka nyumbani wiki mbili zilizo pita
na kwenda kumueleza mwenyekiti wa mtaa
baada ya kuelekezwa ofisi yake ilipo na baada
ya kumueleza hayo alifika nyumbani ndipo nili mwenyekiti aka toa amri ya
kulipwa ujira wangu wote pamoja na kupewa nauli ya kurudi nyumbani kwetu”mwisho wa kunukuu.
Aidha
binti huyo nilipata kuongea nae mambo mengi sana na nikajifunza kuwa kuna
watoto wengi wananyanyaswa sana kwa kivuri cha kufanya kazi za ndani katika
jamii zetu.
Huyu
ni mmoja kati ya mabinti wengi wanao kutana na mikasa kama hiyo na wengine
hukutana na mikasa zaidi ya hii lakini hushindwa kuzitoa sauti zao ili kupewa msaada
zaidi ili kusaidiwa katika mikasa au manyanyaso kama hayo.
Mbali
na manyanyaso hayo baadhi ya waajiri wao wa kiume wamekuwa wakiwahitaji
kimapenzi na pengine hubakwa na waajiri wao na kuwapa vitisho vikali na mabinti
hao huvumilia maana huogopa vitisho hivyo kutokana na umri wao mdogo.
Uelewa
wa mabinti hawa kuwa mdogo na kukosa elimu hushindwa kutoa taarifa kwa majirani
pamoja na mashirika yanayo jihusisha na kutetea haki za wanawake na watoto.
Mashirika
mbalimbali yanayo tete haki za watoto wakishirikiana na jeshi la polisi wamekua
wakitoa elimu juu ya mambo haya na wamekua wakitoa namba zao ili kuwapa taarifa
za mambo kama haya lakini bado jamii haijaamka juu ya manyanyaso kama haya kwa
watoto.
Mgawanyo
wa mwenye nacho na asie kuwa nacho hii inawafanya baadhi yawatu kukjosa utuna
kuwaona binadamu wenzao kama wanyama na kuwafanya unyama kama huo kwa watoto
wasio na hatia.
Sitaki
kuamini kuwa waajiri wote wanao waajiri wa wadada wakazi kuwa wote wana roho za kinyama kiasi hicho bali na
baadhi yao kwasababu kuna wengine ambao huwaajiri watu wazima na kuwalipa ujira
wao vizuri na cha zaidi huushi kama ndugu.
Kilio
cha binti wakazi wa kitanzani nipale anapo kosa haki zake za msingi na hasa
kupewa ujira ambao haulingani na kazi anazopewa pamoja na kunyimwa uhuru wa
kufanya yale anayo yapenda kuyafanya.
Jamii
ielimike na kutambua kuwa kumuajiri mtoto ni kosa la kisheria na mfanya kazi wa
ndani ana haki kama walivyo kua wafanya kazi wengine walivyo na haki wawapo
kazini ikiwemo kupewa ujira unaolingana na kazi wanazo pewa.
Furaha
ya binti wa kazi wa Tanzania ni ni pale tu atakapo wekewa mkataba wa kufanya
kazi, haki zake za msingi pamoja na ujira wenye tija unao lingana na kazi anazo
zifanya.
Mfanya
kazi wa ndani anapaswa kuzijua haki zake za msingingi awapo kazini na pale
anapo ona kuwa anakoasa haki zake za msingingi ni vyema akatoa taarifa katika
vyombo husika ili aweze kusaidiwa haraka iwezekanavyo.
Na
huu ndio mwisho wa makala yetu kwa leo ambapo tumekua tukizungumzia kilio cha
binti wa kazi za ndani wa kitanzania ambapo tumeona changamoto anazo kutana
nazo binti huyu wakazi na kubwa zaidi ikiwa ni kukosa haki zake za msingi.
Nikushukuru
kwa kuchukua muda wako kusoma makala hii naamini umejifunza kitu na utakua
barozi wa kutetea haki za watu hawa kwasababu naamini haya yapo mpaka mtaani
kwako muokoe binti wa kazi za ndani kwa kutoa taarifa katika vyombo husika.
USIKOSE MAKALA IJAYO INAYO HUSU MIMBA ZA UTOTONI
Ø Maana
Ø Chanzo
Ø Madhara
Ø Suruhisho
Ø Maoni
KWA TUKIO AU TANGAZO LOLOTE TUTAFUTE KWA NAMBA. 0713 305 650


0 Maoni