Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea

LONDON.


David de Gea
Arsenal walishambulia lango la Manchester United mara 15 Jumamosi, lakini hawakufanikiwa kutikisa wavu isipookuwa mara moja tu - kikwazo chao David de Gea.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema uchezaji wa golikipa huyo wake ulikuwa "bora zaidi duniani".
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia alikiri kwamba Mhispania huyo alciheza kwa ustadi mkubwa na kwamba "alikuwa ndiye mchezaji bora wa mechi kwa mbali sana".
Uchezaji wake ulikuwa muhimu sana kwani uliwasaidia kulaza Arsenal 3-1 - na pia ulifikia rekodi Ligi ya Premia.
Hatua yake ya kuzima makombora 14 inamfanya kushikilia rekodi ya kuzuia makombora mengi zaidi mechi moja Ligi Kuu England pwa pamoja na mlindalango wa zamani wa Newcastle Tim Krul na kipa wa zamani wa Sunderland Vito Mannone.
Waliozuia makombora mengi zaidi mechi moja EPL tangu Agosti 2003 (Opta walipoanza kufuatilia data)
TareheTimuMchezajiMpinzaniAliokoa
19 Apr 2014SunderlandVito MannoneChelsea14
2 Des 2017Man UtdDavid de GeaArsenal14
10 Nov 2013NewcastleTim KrulTottenham14
21 Mar 2015West BromBoaz MyhillMan City13
7 Nov 2004FulhamMark CrossleyNewcastle13
2 Jan 2017SunderlandVito MannoneLiverpool13
28 Feb 2016SwanseaLukasz FabianksiTottenham13
8 Apr 2006Man CityDavid JamesTottenham13

Chapisha Maoni

0 Maoni