
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema hatua ya rais Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel inaleta wasi wasi katika jitihada za kuleta amani katika mzozo wa Israel na Palestina.
Akizungumza na CNN Guterres ametoa msimamo huo siku ambayo
pia msemaji wa makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameishutumu serikali ya
Palestina.
Msemaji huyo ameongeza hakufurahiswa na kitendo cha rais wa
Palestina Mahmoud Abbas kushindwa kukutana na kiongozi huyo wa Marekani kwa
sababu ya mzozo wa mji wa Jerusalem.
Waandamanaji wameendelea kukusanyika mitaani katika nchi za
Kiaarabu wakipinga hatua hiyo ya raia Trump.
Naye Papa Francis ambaye ni kiongozi wa kidini wa wakatoliki
wapatao billion moja duniani ametoa maoni yake,akisema kuwa Jerusalem ni mji
mtakatifu kwa wakristo,Wayahudi na Waislam.
Amesema ni mazungumzo pekee yanayoweza kuleta suluhu katika
mzozo huo wa Irael na Palestina.

0 Maoni