NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa wakihudumu
katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam.
Miili hiyo
imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.Waliuawawa
wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya
Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini,wanajeshi wengine zaidi ya
50 walijeruhiwa.
Umoja wa
Mataifa ulisema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye
shambulio hilo,waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio hilo.Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alishutumu vikali shambulio hilo na
kusema ni sawa na uhalifu wa kivita.
Aliitaka DR
Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika
wanafaa kuwajibishwa,wanajeshi zaidi walitumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi
cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi. Bw Guterres
alisema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda
amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.


0 Maoni