NA.MWANDISHI
WETU
Waziri mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji
mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.
Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka
3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine.
Aliongea huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa
kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa
Israel.
Ghasia zilizuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na
kwingineno siku ya Jumapili.
Jerusalem kwenyewe, mpalestina mmoja alikamatwa kwa kumdunga
kisu na kumjeruhiwa vibaya afisa wa usalama wa Israel karibu na kituo kimoja
cha basi.
Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa
Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa
wa Jerusalem ni kitu kibaya.
"Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa
Biblia, alisema. Unaweza kuyaskia katika historia ya jamii wa wayahudi kote
duniani… Ni wapi tena kuna mji wa Israel, isipokuwa Jerusalem?
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni