NA.MWANDISHI
WETU
Polisi nchini India wanawahoji
watu kadhaa kufuatia kisa cha ukatili cha ubakaji wa mtoto wa miaka sita katika
jimbo la kaskazini mwa nchi la Haryana.
Mwili wake ulipatikana Jumapili karibu na kwenye nyumba yao
ambapo alidaiwa kutekwa usiku wa tarehe 8 mwezi Disemba.
Kiwango cha majeraha ya mtoto huyo kimewatamausha watu nchini
India,
Mamayake mtoto huyo aliiambia BBC kuwa kile wanataka ni haki.
"Yamepita masaa 24 na bado polisi hajamshika yeyote,"
alisema.
Polisi wamewakamata watu watatuakutoja kwa familia ya mume wake
kuhojiwa lakini hakuna mtu alishikwa hadi sasa.
Serikali imebunia kikosi cha uchunguzi kufuatia shinikizo kutoka
kwa mamlaka ili kuwakamata wale waliotekeleza kitendo hicho.
Wenyeji wakiwemo wanaharakati na viongozi wa kisiasa
wamekusanyika katika kijiji hicho kuandamana.
SOURCE.BBCSWAHILI.COM


0 Maoni