NA.RASHID HASSAN,
WANAKIJIJI
wa mwandege chini,katika kata ya Mwandege wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani,wameillalamikia kampuni ya umeme ya Tanesco kwa kitendo
cha kuweka Transforma karibu na makazi ya watu jambo ambalo limekuwa
likihatarisha maisha ya wanakijiji hicho na kupelekea watu kuzimia,wakati
mwingine watoto huweweseka kutokna na milio ya milipuko inayotokea mara kwa
mara.
Wakazi hao
wakiongea na mwandishi wa plan media wamesema kwamba wamekuwa
wakikosa Amani nyakati ambazo mlipuko wa Transforma hilo unapotokea na
kupelekea matatizo kwa wanakijiji hao kama,watoto zao wanashindwa kusoma kwa
Amani nyakati za usiku,tatizo la moyo kushuka mapigo yake ama kupanda kwa watu
wenye matatizo ya moyo.
Ambapo
wanakijiji hao waliwakilishwa na Ndugu
Said Mkawawa,ambaye alisema ni kweli tatizo ni kubwa na wao ndio
waathirika wakubwa na amewataka wahusika kuwasaidi haraka iwezekanavyo ili
kuwapa Amani ya kuishi pasipo kubugudhiwa na jambo lolote ili kila mmoja afanye
jukumu linalomhusu na kwa wakati sahihi.
Katika
juhudi za mwandishi wa plan media,alifanikiwa kuongea na mjumbe wa kijiji
hicho Bwana[ Ally Hemedi alisema kuwa jambo hilo ni la mda mrefu limekuwa
likiwakwaza wanakijiji wake ila juhudi alizotumia ni kubwa ambapo mwanzo
lilikuwa nyuma ya nyumba ya mmoja wa wakazi hao lakini baada ya malalamiko
limesogezwa mbelekidogo ambapo bado limekuwa ni tatizo kwa wanakijiji hao.
Katika
juhudi zilizofanywa na mwandishi wa plan media za kuwatafuta wahusika wakuu
wanaolalamikiwa ambao ni Tanesco ya wilaya ya mkulanga zilishindikana juhudi za
kuwapata kutokana na mambo yaliyo nje na uwezo wetu,lakini rai ya wanakijiji
hao wameiomba kampuni hiyo kushughulikia jambo hilo haraka iwezekanavyo.

0 Maoni