NA.MWANDISHI WETU
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Butiama mkoani Mara Solomoni Ngiliule kuanzia leo
kutokana na ubadhirifu wa fedha za Umma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo ameyasema
maamuzi hayo leo tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi
kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Butiama.
SOURCE.BONGO 5.COM


0 Maoni