NA.GOODLUCK CHRISTOPHER
Muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania Baisa Mhela
aendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa baada ya kupokelewa vyema
katika mji wa Mombasa nchini Kenya ambapo amekua na tamasha kubwa la fungua
mwaka 2018.
Aidha muimbaji huyo amepata nafasi ya kuendelea
kufanya matamasha mbalimbali ambapo anatarajia kufanya tamasha kubwa sana
mapema mwezi wapili kwaka 2018 katika mji wa Mombasa nchini Kenya.
Vilevile Baisa amesema kuwa anafurahia mapokezi
mazuri kwa wakazi wa Mombasa ambapo hivi sasa anaishi na wenyeji kama mzawa
ikiwa ni tofauti na mwanzo ambapo alikua akilala kwenye hoteli jambo ambalo
lilikua linamgharimu kiasi kikubwa cha pesa.
Hata hivyo Baisa ameahidi mambo mazuri kutoka Kenya kiwemo
kufanya video ya wimbo wake mpya wa JUST, kufanya wimbo mpya kwa kumshirikisha
msanii kutoka nchini Kenya pamoja na kuingia mikataba na kampuni kadhaa ambapo
ataweka bayana hapo baadae kidogo mambo yakisha kamilika.
Baisa amemaliza kwa kuwaomba wau wadau wa muziki wa
injili kuendelea kumuombea pamoja na kufuailia kazi zake ikiwemo nyimbo zake
kwa utukufu wa Mungu ili kuikuza huduma yake ya kuihubiri injili kwa njia ya
nyimbo kwa mataifa zaidi ya alipo fikia sasa.
TANGAZA NA PLANMEDIA LEO:
+255 713 305 650
planmediatz@gmail.com


0 Maoni