NA.GOODLUCK CHRISTOPHWER
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dkt. Harrison Mwakyembe hapo jana( Jumapili) alikwenda kumtembelea msanii wa
filamu Bongo, Wastara Juma nyumbani kwake na kumjulia hali.
Mh.Waziri Mwakyembe ambaye aliambata na Katibu wa Bodi ya Filamu walifika nyumbani kwa muigizaji huyo kwa ajili ya kumjulia hali ambapo Waziri huyo aliahidi kumsaidia kiasi cha shilingi milioni1 kwa ajili kwenda India kwa ajili ya matibabu yake.
Hata hivyo Waziri Mwakyembe
amewaomba wasanii wote nchini kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia Wastara
Juma ambae anahitaji kiasi cha shilingi milioni37, kwa ajili ya kurudi katika
hospitali aliyokuwa akitibiwa hapo awali .
Kitendo cha Mh,Waziri
kufika nyumbani kwa muigizaji huyo kimekuja baada ya msanii huyo kuomba msaada
kutokana na hali yake hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki miaka kadhaa
iliyopita na kumsababisha kukatwa mguu.


0 Maoni