Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AGEUKIA KILIMO

NA,GOODLUCK CHRISTOPHER
Msanii chipukizi wa nyimbo za kumsifu mungu[injili]nchini Tanzani a anaefahamika kwa majina ya Betha Mwafilombe,amevunja ukimya kwa kusema anajishughulisha na kilimo cha mpunga lengo lake likiwa ni kujihimalisha kifedha ili kufikisha muziki wake mbali.

Hayo ameyasema alipokuwa  akizungumza na Plan Media katika mahojiano ya hivi  karibuni yaliyofanyika kwa njia ya simu.

Changamoto kubwa anayo kutana nayo kwasasa ni ukosefu wa soko la kudumu la kuuzia kazi zake zilizo kwenye mfumo wa CD ambapo jambo hilo limekuwa tatizo kutokana na utandawazi wa watu kunyonya  vitu mitandaoni kwa kutumia simu  na kiamba mpakato[computer].

 Betha anatarajia kufanya uzinduzi wa albam yake mpya inayo kwenda kwajina la kwa Neema ndani ya mwaka huu mala baada ya kukamilisha taratibu zote na kutaja kuwa utakua uzinduzi wa historia katika taifa la Tanzania.

Amemaliza kwakuomba ushirikiano kutoka kwa mashabiki wa kazi zake kwa mchango wa pesa au mawazo ili kuisogeza huduma yake kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Kwa mahitaji ya CD  Piga namba +255 713 305 650

Chapisha Maoni

0 Maoni