|
NA.RASHID HASSAN
Kumbilamoto aziita kampeni za wapinzani
sarakasi za usiku. MGOMBEA ngazi ya Diwani kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM ,Omary Said Kumbilamoto, amesema kwamba kampeni zinazofanywa na wapinzani
wake ni sawa na sarakasi za usiku ambazo hazionekani mpaka ziwashiwe taa.
Amesema kwamba wapinzani hao wamekuwa
wakitumia mgongo wake katika kuomba kura kwa wana nchi jambo ambalo
amelifananisha na sarakasi za usiku ambapo zikiwashwa taa ndio zinaonekana
"" Hawa jamaa zangu ni watu wa ajabu sana, kwa sasa hawana jipya
kwani kilichobakia ni siasa za sarakasi, Mimi ni taa hivyo hawawezi kuonekana
mpaka niwake hivyo sitojali na watazidi kupata tabu sana na Mimi"amesema
Kumbilamoto.
[pichani ni Ndugu Omary Said Kumbilamoto akitoa sera zake mbele ya wananchi waliohudhuria kwenye viwanja vya shule ya KOMBOvilivyopo vingunguti}.
Aidha, amewaomba wakazi wa Vingunguti
wasitishike na vitisho vyao kwani wanatapatapa hawana njia ya kujificha. Pia
amewaomba wazidi kumjengea imani ili wamchague tena kwa ajili ya
kuwatumikia wana nchi hao kwani chama alichokuwa nacho kwa sasa kinatekeleza
ilani na Sera zake zinaeleweka.
Naye Mbunge wa Jimbo la Segerea , Bonnah Kaluwa, amewaomba wana nchi wamchague
Kumbilamoto ili hata yale mambo yaliyokuwa yakishindikana kupitia Baraza LA
madiwani yaweze kupita kwa urahisi. " Jimbo langu hakuna hata
mwakilishi kutoka chama cha CCM, hivyo mkiniletea Kumbilamoto mtanirahisishia
kazi.
[Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mh Bonna Kaluwa akinadi sera za mgombea udiwani kupitia chama cha Ccm ,Picha na Rashid Hassan.]
Mbali na hayo, amesema mpaka sasa Serikali
imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kufanya upanuzi wa zahanati ya
Mnyamani kuwa kituo cha afya.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa
mwanachama wa Chadema ambaye alikuwa katika ngazi mbali mbali
ikiwamo mkuu wa Idara ya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es Salaam.
Pamoja
na mwenyekiti wa Jimbo La uchaguzi Ukonga, Kidera Gango, amesema kauli za
wapinzani za kusema wamenunuliwa zipuuzwe kwamba wao walijiondoa kuunga
juhudi za Mh Rais Magufuli" Kweli tumenunuliwa lakini sio kwa fedha,
kununuliwa kwetu kumetokana na Sera nzuri za CCM pamoja na ilani yake inayotekelezeka"amesema
Gango
Pia amesema kwamba, ccm ni chama pekee
chenye ilani na kwamba vyama vingine viliungana na kujitengenezea karatasi
zenye malalamiko huku wakiziita ni Sera zao
|

0 Maoni