Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

VIGOGO WAZIDI KUCHAGIZA USHINDI WA KUMBILAMOTO.

NA,RASHID HASSAN
Shamra shamra za Kampeni zikizidi kunoga na kuelekea tamati , leo tumeshuhudia baadhi ya Vigogo wakubwa wenye nyadhifa CCM , wakijitokeza kwa wingi kumnadi Mgombea ngazi ya Udiwani aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto katika Kampeni za kutetea kiti chake kupitia CCM.
Miongoni Mwa Vigogo waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Wazazi Taifa , Dr Edmund Bernard Mndolwa, Katibu wa Wazazi Taifa Ndugu Erasto Sima, Sangara Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Segerea Mh: Bonnah Kaluwa , Mbunge wa Ilala , Mh Zungu, Julius Mtatiro aliyetoka CUF pamoja na Viongozi wa ngazi mbalimbali.
 Katika kuona Ccm inapata ushindi, Mgeni rasmi Edmund Bernard Mndolwa, amesema huu ndio wakati wao wa kumchagua Kumbilamoto kuwa Diwani wao ili akashirikiane vema na Serikali katika kutatua Kero za Wananchi.

 Pia amesema Omary ni mchapakazi na wao kama chama hawakufanya makosa kumpisha Kumbilamoto kwani wanajua kero zitataturika kwa haraka tofauti na alivyokuwa upinzani . " Niwaambie kitu, Sera za wapinzani ni kutofanya kazi na serikali , sasa kama huwashirikishi hao maendeleo yatakujaje? Sasa msifanye makosa tuleteeni Kumbilamoto Vingunguti mfaidi matunda

 Katika hatua nyingine , Mbunge wa Ilala Mh Zungu, amesema kuwa ccm hawanunui kura wala watu Bali wanashinda kwa ajili ya kuwajali watu.
 
 Amesema kuwa wao kama chama hawachagui watu kwa ajili ya kuuza sura , wanachokiangalia ni uwajibikaji na kujali kero za wananchi. Pia amewataka wakazi hao kumchagua Kumbilamoto kwani tayari ameshawasiliana na viongozi wa Serikali TAMISEMI pamoja na Waziri wa Maji na Ujenzi watakwenda Vingunguti wiki ijayo ili kutatua kero katika sekta hizo alizo zitaja. Hata hivyo , Julius Mtatiro, amesema kuwa chama cha CUF kimeguka vipande vipande hivyo aliona ni vyema akatafuta jukwaa sahihi la kutatua kero za wananchi na maskini ambapo ni CCM.

Amesema kabla ya Kumbilamoto kujinga na ccm, alikuwa kiongozi pekee wa udiwani mchapakazi kuliko Madiwani wote wa upinzani. " Ndugu zangu nimekaa CUF miaka 10, miaka yote niliyokuwepo sijaona mafanikio zaidi ya migogoro, Sasa nikiongeza miaka 10 mingine nitapoteza uelekeo wangu wa Kisiasa njia sahihi nikajiunga na CCM kwa matakwa yangu binafsi na wala sijanunuliwa kama Maneno yanavyozidi kusemwa "amesema Mtatiro.

Naye Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa, amewaomba wakazi wa Vingunguti wampatie Kumbilamoto kwani katika Jumbo lake hakuna mtu wa ccm hivyo ni vigumu kupitisha bajeti za maendeleo mbele ya wapinzani. Katika hayo, Mgombea Udiwani Kumbilamoto , ameomba kura zake huku akizidi kuwaahidi wananchi wake maisha bora watakapo mchagua tena

 

Chapisha Maoni

0 Maoni