Na,Goodluck Christopher
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda amessisitiza swala la Usafi kwa wakazi wa jiji hilo huku akisema kuwa kwa kufanya hivyo kutapunguza magonjwa yamlipuko kama vile Marelia na U.i.t.
Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Anatoglo ambapo amezishukuru kampuni binafsi kwa kushirikiana na na serikali katika swala zima la usafi, huku akisema kampuni zote zilizodanganya katika swala hilo la usafi atazishughurikia.
Pia amesema kuwa tangu ianze kampeni ya Usafi takribani watu 11,669 wamekamatwa, 6, 577 wamepigwa faini, 4,443 waliachiwa, 3,76 walidhaminiwa na ndugu Zao, 6 walipelekwa mahakamani, 2,213 adhabu ya usafi na takribani milioni mia tatu arobaini na sita elfu na laki sita zimekusanywa kutokana na makosa ya usafi.
Lakini pia Paul Makonda amelaani vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wanamgambo ambao wanachukuwa sheria mkononi kwa kuwapiga raia hivyo wanapaswa kuwakamata na kuwapeleka kwenye vituo husika na si vinginevyo.
Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa Abubakari Musa amesema kuwa Usafi ni Uhai hivyo amewaomba wananchi kwa pamoja kushirikiana ili kulipa heshima jiji la Dar es salaam pamoja na kupunguza magonjwa yanayotokana na uchafu


0 Maoni