Mwafrika Digital

https://youtu.be/ArXfq-5TVWA Subscribe Mwafrika TV

CCM YAVUNJA NGOME YA CUF


NA, RASHID HASSAN
CCM yabomoa ngome ya CUF, Kumbilamoto asema bado Picha kamili. KAMPENI za Udiwani zimeendelea Leo Kata ya Vingunguti, huku tukishuhudia Ngome ya CUF ikizidi kumeguka vipande vipande hii ni Mara baada ya Viongoz wa juu kurudisha kadi zao na kujiunga CCM.
Akizungumza katika Kampeni hizo, Julius Mtatiro, amesema kwamba chama cha CUF inatafunika vipande vipande kwa ajili ya ubinafsi wa vyama vya upinzani huku kikikosa muelekeo.

 Amesema kuwa wato hao wamejiunga na CCM kumfuata Kumbilamoto kutokana na madudu yanayofanywa na chama hicho .
Pia amesema kuwa ,  mwaka  2011, CUF kilifanikiwa kuwa na wabunge 2 kwa Tanzania bara na zaidi ya madiwani 200.

Hata hivyo amesema mwaka  2015 CUF ilipata jumla ya madiwani 400 na kufanikiwa kuongoza Halmashauri ambapo ni mabadiliko makubwa ndani ya chama hicho kilichokuwa kina wasomi wachache na kupambana kupata wasomi.


Amesema Vyama vya upinzani havina malengo ya muda mrefu kwani akili  zao zimeegemea na kulenga kupata wabunge na madiwani bila ya kuwa na mipango ya kisiasa.
 Hivyo amesema Madiwani wengi na wabunge wa CUF watajiondoa huko kutokana na sarakasi zinazoendelea na ukosefu wa muelekeo wa kisiasa.

 Wakati huo huo akieleza mustakabadhi wa vijana, amesema Vijana wengi wanaingia katika majukwaa ya kisiasa kwa ajili ya kutafuta fursa za kutumikia kwa vipawa vyao katika kutafuta mbinu mbadala za kutatua kero na kupambana na umasikini. " Lazima niwe mkweli, nchi hii ikifikia wakati watu wenye  Pesa hawashikiki , Leo Rsis Magufuli amewatuliza na amerejesha Heshima ya Taifa hili LA masikini na Wanyonge Sasa utashindwaje kuunga mkono?  Halafu upinzani tunapinga "amesema Mtatiro.

Serikali ya awamu ya tano tangia iingie madarakani kuna Mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo, hivyo ili ufanye kazi vizuri na kuitendea haki nafasi yako Hamis CCM utakuwa huru .
Naye Omary Kumbilamoto, amesema yeye siye  mzungumzaji sana Bali yupo katika kusimamia Yale anayoyaahidi kwa vitendo. Hivyo amewaomba wana Vingunguti wasifanye makosa wazidi kumuamini ili azidi kuwatimizia Yale wananchi wanayoyataka na kuyaahidi katika utatuzi wa kero. "Ndugu zangu nataka kuwaambia hii Picha iliyojitokeza Leo ni kisanga kikubwa bado mafuriko yanakuja hivyo wale mliobakia CUF rudini nyumbani kumenoga" amesema Kumbilamoto.

Mbali na Kumbilamoto, aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mtakuja, Ndugu Sharif Mbulu, amesema kuhama kwake chama kumetokana na mgogoro unaoendelea CUF , hivyo ameipongeza Kamati kuu  ya CCM kwa kumpokea vizuri na yupo tayari kushirikiana nao. 
"Nimeachia nyadhifa zangu zote zikiwemo za Serikali na kujiunga CCM, Mimi sio mjinga nimepima kina cha Maji nikaona siwezi kuyavamia na nimeungana na Ndugu yangu Kumbilamoto kwani ameniachia majukumu mwezi sasa sitoki nje nawaza kuwajibu wana Vingunguti kwanini Kumbilamoto amehama  CUF" amesema Mbulu.



Chapisha Maoni

0 Maoni