Na:Rashid Hassan
KATIBU ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA Humphrey Pole pole, amefunga Kampeni ya ugombea Udiwani kata ya Vingunguti Leo kama mgeni rasmi huku akizidi kuwaachana wapinzani akisema wamepoteza muelekeo wa kisiasa.

Amesema kwamba , Wapinzani kwa sasa wamebaki kukurupuka na kutengeneza majungu huku wao wakizidi kuwa ngangari na wanasonga mbele.
Amesema tayari Serikali imetenga Pesa takribani Bilioni 4 kwa ajili ya kukopeshwa Vijana, Wazee, Waremavu pamoja na wakina Mama bila riba.
Pia katika kuona kero ya Maji Vingunguti inakuwa historia, tayari wameshafanya mazungumzo na DAWASA hivyo kilichobakia ni utekelezaji ambao muda wowote unaweza kuanza kutandaza Mabomba kwenye Kata hiyo. Katika maboresho ya Elimu, amesema tayari Serikali imetenga kiasi cha Milioni 150, kwa ajili ya kuziingiza kwenye kamati za shule za Msingi ambazo zimechakaa kuanza ukarabati Mara moja.

"Wapo wapinzani wao hawaoni kinachofanywa na Serikali hii kazi yao ni kupinga tuu, lakini nataka kuwaambieni sisi hatuwajibu kwa maneno bali tunawajibu kwa vitendo hadi wenzao wanawatoroka hadi 2020 upinzani utabakia historia" Amesema Pole Pole.
Naye Mgombea wa Udiwani wa Vingunguti , Omary Said Kumbilamoto ,yeye hakuwa na Maneno mengi alichowaomba ni kumchagua awafanyie maendeleo.
" Leo sina mengi niliyoyafanya na ninayoendelea kuyafanya vinatosha kunipa kura nawaombeni msifanye makosa nimerudi nyumbani naombeni kura za ndio kesho asanteni sana kwa kuja Mungu awabariki sana"
Amesema Kumbilamoto. Katika hatua nyingine, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Buguruni kwa Mnyamani tiketi ya CUF, Mh: Shukuru Dege, amejiunga na CCM Leo Mara baada ya kurudisha kadi mbele ya Pole Pole.
Dege amesema kuwa amekaa CUF tangia mwaka 1992 lakini hajaona lamaana baada ya kuona chama chake kikipoteza muelekeo.
Amesema hakuna vyama vya siasa , bali kuna genge la watu furani walio jitengenezea utaratibu wa kula ruzuku za Serikali. Amesema CUF mgogoro mkubwa ni kugombea ruzuku ya milioni 160. "
Ninayo mengi ya kusema kwa vile hapa sio mahala pake na nimepewa muda mchache nitatafuta muda ni zungumze nawaombeni wakazi wa Vingunguti kesho mpigieni kura Kumbilamoto kwani ni mchapakazi "Amesema Dege.

0 Maoni